Colossians 3:13 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Vumilianeni na kusameheana iwapo mmoja wenu analo jambo lolote dhidi ya mwenzake. Mnapaswa kusameheana kama Bwana alivyowasamehe nyinyi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Vumilianeni na kusameheana mtu akiwa na lalamiko lolote dhidi ya mwenzake. Sameheaneni kama vile Bwana Isa alivyowasamehe ninyi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
mkichukuliana, na kusameheana, mtu akiwa na sababu ya kumlaumu mwenzake; kama Bwana alivyowasamehe ninyi, vivyo na ninyi.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Msikasirikiane, bali msameheane. Mtu yeyote akikukosea, msamehe. Wasameheni wengine kwa sababu Bwana amewasamehe ninyi.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Vumilianeni na kusameheana iwapo mmoja wenu analo jambo lolote dhidi ya mwenzake. Mnapaswa kusameheana kama Bwana alivyowasamehe ninyi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Vumilianeni na kusameheana iwapo mmoja wenu analo jambo lolote dhidi ya mwenzake. Mnapaswa kusameheana kama Bwana alivyowasamehe nyinyi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Vumilianeni na kusameheana. Mtu akiwa na lalamiko lo lote dhidi ya mwenzake, sameheaneni kama vile Bwana alivyowasamehe ninyi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Vumilianeni na kusameheana mtu akiwa na lalamiko lolote dhidi ya mwenzake. Sameheaneni kama vile Bwana Isa alivyowasamehe ninyi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
mkichukuliana, na kusameheana, mtu akiwa na sababu ya kumlaumu mwenzake; kama Bwana alivyowasamehe ninyi, vivyo na ninyi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Vumilianeni na kusameheana iwapo mmoja wenu analo jambo lolote dhidi ya mwenzake. Mnapaswa kusameheana kama Bwana alivyowasamehe nyinyi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mvumiliane ninyi kwa ninyi na kuachiliana, mtu akiwa na neno la kumkamia mwenziwe! Kama naye Bwana alivyowaachilia ninyi, vivyo hivyo vifanyeni nanyi!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
mkichukuliana, na kusameheana, mtu akiwa na sababu ya kumlaumu mwenzake; kama Bwana alivyowasamehe ninyi, vivyo na ninyi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Muvumiliane na kusameheana ninyi kwa ninyi wakati wowote mutu anapokuwa na neno la kumushitaki mwingine. Munapaswa kusameheana kama vile Bwana alivyowasamehe ninyi.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
mkichukuliana, na kuachiliana, mtu akiwa na sababu ya kumlaumu mtu; jinsi Kristo alivyowaachilieni, vivyo hivyo na ninyi.