Colossians 3:14 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Zaidi ya hayo yote, zingatieni upendo, kwani upendo huunganisha kila kitu katika umoja ulio kamili.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Zaidi ya maadili haya yote jivikeni upendo, ambao ndio unaofunga kila kitu pamoja katika umoja mkamilifu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Zaidi ya hayo yote jivikeni upendo, ndio kifungo cha ukamilifu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Pamoja na haya yote, vaeni upendo. Upendo ndicho kitu kinachounganisha kila kitu katika umoja mkamilifu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Zaidi ya hayo yote, zingatieni upendo kwani upendo huunganisha kila kitu katika umoja ulio kamili.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Zaidi ya hayo yote, zingatieni upendo, kwani upendo huunganisha kila kitu katika umoja ulio kamili.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Zaidi ya maadili haya yote jivikeni upendo, ambao ndio unaofunga kila kitu pamoja katika umoja mkamilifu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Zaidi ya maadili haya yote jivikeni upendo, ambao ndio unaofunga kila kitu pamoja katika umoja mkamilifu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Zaidi ya hayo yote jivikeni upendo, ndio kifungo cha ukamilifu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Zaidi ya hayo yote, zingatieni upendo, kwani upendo huunganisha kila kitu katika umoja ulio kamili.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini lililo kuu kuliko haya yote: uvaeni upendano! Maana ndio unaoyatimiza yote na kutupatanisha kuwa mmoja.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Zaidi ya hayo yote jivikeni upendo, ndio kifungo cha ukamilifu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Zaidi ya mambo haya yote, mukuwe na upendo, maana upendo unaunganisha kila kitu katika umoja unaokuwa mukamilifu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Juu ya haya yote vaeni upendo, ndio kifungo cha ukamilifu.