Colossians 3:15 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nayo amani ya Kristo itawale mioyoni mwenu; maana kwa ajili hiyo nyinyi mmeitwa katika mwili huo mmoja. Tena muwe na shukrani!
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Amani ya Al-Masihi na itawale mioyoni mwenu, kwa kuwa ninyi kama viungo vya mwili mmoja mmeitiwa amani. Tena kuweni watu wa shukrani.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na amani ya Kristo iamue mioyoni mwenu; ndiyo mliyoitiwa katika mwili mmoja; tena iweni watu wa shukrani.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Amani inayotoka kwa Kristo itawale fahamu zenu. Mliitwa kwa ajili ya amani ili muwe pamoja katika mwili mmoja. Mwe na shukrani daima.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Nayo amani ya Kristo itawale mioyoni mwenu; maana kwa ajili hiyo ninyi mmeitwa katika mwili huo mmoja. Tena muwe na shukrani!
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nayo amani ya Kristo itawale mioyoni mwenu; maana kwa ajili hiyo nyinyi mmeitwa katika mwili huo mmoja. Tena muwe na shukrani!
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Amani ya Kristo na itawale mioyoni mwenu, kwa kuwa ninyi kama viungo vya mwili mmoja mmeitiwa amani. Tena iweni watu wa shukrani.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Amani ya Al-Masihi na itawale mioyoni mwenu, kwa kuwa ninyi kama viungo vya mwili mmoja mmeitiwa amani. Tena kuweni watu wa shukrani.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na amani ya Kristo iamue mioyoni mwenu; ndiyo mliyoitiwa katika mwili mmoja; tena iweni watu wa shukrani.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nayo amani ya Kristo itawale mioyoni mwenu; maana kwa ajili hiyo nyinyi mmeitwa katika mwili huo mmoja. Tena muwe na shukrani!
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nao utengemano wa Kristo utawale mioyoni mwenu! Kwani ndio, mlioitiwa, maana m mwili mmoja. Tena mema, mliyogawiwa, myavumishe!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na amani ya Kristo iamue mioyoni mwenu; ndiyo mliyoitiwa katika mwili mmoja; tena iweni watu wa shukrani.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Amani ya Kristo itawale katika mioyo yenu; maana ni kwa ajili ya hiyo ninyi mumeitwa kuwa katika mwili mumoja. Mukuwe wenye shukrani.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Na amani ya Mungu iamue mioyoni mwenu, ndiyo mliyoitiwa katika mwili mmoja; na mwe watu wa shukrani.