Colossians 3:22 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Enyi watumwa, watiini wakuu wenu wa kidunia katika mambo yote, na si tu wakati wanapowatazama kwa kuwa mnataka kujipendekeza kwao; ila fanyeni hivyo kwa moyo wote, kwa sababu ya kumcha Bwana.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ninyi watumwa, watiini mabwana zenu wa hapa duniani katika mambo yote. Fanyeni hivyo si wakiwepo tu, wala si kwa kujipendekeza tu kwao, bali kwa moyo mnyofu na kumcha Bwana.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ninyi watumwa, watiini hao ambao kwa mwili ni bwana zenu, katika mambo yote, si kwa utumwa wa macho, kama wajipendekezao kwa wanadamu, bali kwa unyofu wa moyo, mkimcha Bwana.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Enyi watumwa, watiini mabwana zenu katika mambo yote. Mwe watii kila wakati, hata kama wao hawawezi kuwaona. Msijifanye kazi kwa bidii ili wawatendee mema. Mnapaswa kuwatumikia mabwana zenu kwa moyo kwa sababu mna hofu ya Bwana.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Enyi watumwa, watiini wakuu wenu wa kidunia katika mambo yote, na si tu wakati wanapowatazama kwa kuwa mnataka kujipendekeza kwao; ila fanyeni hivyo kwa moyo wote, kwa sababu ya kumcha Bwana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Enyi watumwa, watiini wakuu wenu wa kidunia katika mambo yote, na si tu wakati wanapowatazama kwa kuwa mnataka kujipendekeza kwao; ila fanyeni hivyo kwa moyo wote, kwa sababu ya kumcha Bwana.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ninyi watumwa, watiini mabwana zenu wa hapa duniani katika mambo yote. Fanyeni hivyo si wakiwepo tu, bali mkimwogopa Mungu, wala si kwa kutafuta upendeleo wao wakati wanapowaona.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ninyi watumwa, watiini mabwana zenu wa hapa duniani katika mambo yote. Fanyeni hivyo si wakiwepo tu, wala si kwa kutafuta upendeleo wao, bali kwa moyo mnyofu na kumcha Bwana Isa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ninyi watumwa, watiini hao ambao kwa mwili ni bwana zenu, katika mambo yote, si kwa utumwa wa macho, kama wajipendekezao kwa wanadamu, bali kwa unyofu wa moyo, mkimcha Bwana.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Enyi watumwa, watiini wakuu wenu wa kidunia katika mambo yote, na si tu wakati wanapowatazama kwa kuwa mnataka kujipendekeza kwao; ila fanyeni hivyo kwa moyo wote, kwa sababu ya kumcha Bwana.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ninyi watumwa, katika mambo yote watiini walio mabwana zenu kimtu! Msiwatumikie hapo machoni tu, kama wenye kupendeza watu, ila kama wenye kumwogopa Bwana watumikieni kwa mioyo iliyo na neno moja tu!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ninyi watumwa, watiini hao ambao kwa mwili ni bwana zenu, katika mambo yote, si kwa utumwa wa macho, kama wajipendekezao kwa wanadamu, bali kwa unyofu wa moyo, mkimcha Bwana.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ninyi watumwa, muwatii wabwana wenu katika mambo yote hapa katika dunia. Musiwatii tu wakati wanapowaangalia ninyi kama mungetaka tu kujipendeza mbele yao, lakini muwatii kwa moyo mwema, kwa sababu munamuheshimu Bwana.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Ninyi watumwa, watiini wao ambao kwa niwili ni bwana zenu, katika mambo yote, si kwa utumwa wa macho, kama wajipendekezao kwa wana Adamu, bali kwa unyofu wa moyo, mkimeha Mungu.