Colossians 3:8 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini sasa mnapaswa kuachana na mambo haya yote: Hasira, tamaa na uovu; kufuru au maneno yasiyofaa yasitoke kamwe vinywani mwenu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini sasa yawekeni mbali nanyi mambo kama haya yote: yaani hasira, ghadhabu, uovu, masingizio na lugha chafu kutoka midomoni mwenu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini sasa yawekeni mbali nanyi haya yote, hasira, na ghadhabu, na uovu, na matukano, na matusi vinywani mwenu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Lakini sasa, jitengeni mbali na mambo haya katika maisha yenu: hasira, ukorofi, chuki, na mazungumzo yenye matusi.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Lakini sasa mnapaswa kuachana na mambo haya yote: hasira, tamaa, uovu; kufuru au maneno yasiyofaa yasitoke kamwe vinywani mwenu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini sasa mnapaswa kuachana na mambo haya yote: hasira, tamaa na uovu; kufuru au maneno yasiyofaa yasitoke kamwe vinywani mwenu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini sasa yawekeni mbali nanyi mambo kama haya yote, yaani: Hasira, ghadhabu, uovu, masingizio na lugha chafu kutoka midomoni mwenu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini sasa yawekeni mbali nanyi mambo kama haya yote: yaani hasira, ghadhabu, uovu, masingizio na lugha chafu kutoka midomoni mwenu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini sasa yawekeni mbali nanyi haya yote, hasira, na ghadhabu, na uovu, na masuto, na matusi vinywani mwenu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini sasa mnapaswa kuachana na mambo haya yote: Hasira, tamaa na uovu; kufuru au maneno yasiyofaa yasitoke kamwe vinywani mwenu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini sasa nanyi hayo yote sharti myatoke: makali na mifundo ya mioyo na maovu na matusi na mateto mabaya yaliyomo vinywani mwenu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini sasa yawekeni mbali nanyi haya yote, hasira, na ghadhabu, na uovu, na matukano, na matusi vinywani mwenu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini sasa mutupilie mbali mambo haya yote: kasirani, chuki, uovu, masingiziano na musiseme neno lolote baya.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Lakini sasa yawekeni mbali haya yote, hasira, na ghadhabu, na uovu, na matukano, na matusi vinywani mwenu.