Colossians 4:10 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Aristarko, ambaye yuko kifungoni pamoja nami, anawasalimuni; hali kadhalika Marko, binamu yake Barnaba, (mmekwisha pata maagizo juu yake; akifika kwenu mkaribisheni).
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Aristarko aliye mfungwa pamoja nami anawasalimu, vivyo hivyo Marko, binamu yake Barnaba. (Mmeshapata maagizo yanayomhusu; akija kwenu, mpokeeni.)
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Aristarko, aliyefungwa pamoja nami, awasalimu; na Marko, mjomba wake Barnaba, ambaye mmepokea maagizo kwa habari yake; akifika kwenu mkaribisheni.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Aristarko, aliyefungwa pamoja nami humu gerezani anawasalimu. Marko, binamu yake Barnaba anawasalimu pia. (Nimekwisha kuwaambia kuhusu Marko. Ikiwa atakuja, mpokeeni.)
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Aristarko, ambaye yuko kifungoni pamoja nami, anawasalimuni; hali kadhalika Marko, binamu yake Barnaba, (mmekwisha pata maagizo juu yake; akifika kwenu mkaribisheni).
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Aristarko, ambaye yuko kifungoni pamoja nami, anawasalimuni; hali kadhalika Marko, binamu yake Barnaba, (mmekwisha pata maagizo juu yake; akifika kwenu mkaribisheni).
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Aristarko aliye mfungwa pamoja nami anawasalimu, vivyo hivyo Marko, binamu yake Barnaba. (Mmeshapata maagizo yanayomhusu; akija kwenu, mpokeeni).
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Aristarko aliye mfungwa pamoja nami anawasalimu, vivyo hivyo Marko, binamu yake Barnaba. (Mmeshapata maagizo yanayomhusu; akija kwenu, mpokeeni.)
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Aristarko, aliyefungwa pamoja nami, awasalimu; pamoja na Marko, binamu yake Barnaba, ambaye mmepokea maagizo juu yake; akifika kwenu mkaribisheni.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Aristarko, ambaye yuko kifungoni pamoja nami, anawasalimuni; hali kadhalika Marko, binamu yake Barnaba, (mmekwisha pata maagizo juu yake; akifika kwenu mkaribisheni).
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Aristarko, mfungwa mwenzangu, na Marko, mpwae Barnaba, wanawasalimu ninyi; kwa ajili yake yeye mmepata maagizo; atakapokuja kwenu, mpokeeni!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Aristarko, aliyefungwa pamoja nami, awasalimu; na Marko, mjomba wake Barnaba, ambaye mmepokea maagizo kwa habari yake; akifika kwenu mkaribisheni.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mufungwa mwenzangu Aristarko anawasalimia. Naye Marko, binamu wa Barnaba anawasalimia vilevile. (Mumekwisha kupata maagizo juu ya Marko; akifika kwenu mumupokee vizuri).
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Aristarko, aliyefumgwa pamoja nami, awasalimu, na Marko, mjomba wake Barnaba, amhae mmepokea maagizo kwa khabari yake; akifika kwenu mkaribisheni.