Colossians 4:11 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Naye Yoshua aitwaye Yusto, anawasalimuni. Miongoni mwa Wayahudi waliokwisha pokea imani, hawa tu peke yao, ndio wanaofanya kazi pamoja nami kwa ajili ya ufalme wa Mungu; nao wamekuwa msaada mkubwa kwangu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Isa aitwaye Yusto pia anawasalimu. Hawa peke yao ndio Wayahudi miongoni mwa watendakazi wenzangu kwa ajili ya ufalme wa Mungu, nao wamekuwa faraja kwangu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na Yesu aitwaye Yusto; hao ni watu wa tohara. Tena hao peke yao ni watendaji wa kazi pamoja nami kwa ajili ya ufalme wa Mungu; nao walikuwa faraja kwangu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Pia pokeeni salamu toka kwa Yesu, aitwaye pia Yusto. Hawa ni Wayahudi waamini pekee wanaofanya kazi pamoja nami kwa ajili ya ufalme wa Mungu. Wamekuwa faraja kubwa sana kwangu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Naye Yoshua aitwaye Yusto, anawasalimuni. Miongoni mwa Wayahudi waliokwisha pokea imani, hawa tu peke yao, ndio wanaofanya kazi pamoja nami kwa ajili ya Utawala wa Mungu; nao wamekuwa msaada mkubwa kwangu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Naye Yoshua aitwaye Yusto, anawasalimuni. Miongoni mwa Wayahudi waliokwisha pokea imani, hawa tu peke yao, ndio wanaofanya kazi pamoja nami kwa ajili ya ufalme wa Mungu; nao wamekuwa msaada mkubwa kwangu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Yesu, yeye aitwaye Yusto, pia anawasalimu. Hawa peke yao, ndio Wayahudi miongoni mwa watenda kazi wenzangu kwa ajili ya Ufalme wa Mungu, nao wamekuwa faraja kwangu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Isa, yeye aitwaye Yusto, pia anawasalimu. Hawa peke yao ndio Wayahudi miongoni mwa watendakazi wenzangu kwa ajili ya Ufalme wa Mwenyezi Mungu, nao wamekuwa faraja kwangu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na Yesu aitwaye Yusto awasalimu. Hao tu ndio watu wa tohara miongoni mwa wale watendao kazi pamoja nami kwa ajili ya ufalme wa Mungu; nao wamekuwa msaada kwangu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Naye Yoshua aitwaye Yusto, anawasalimuni. Miongoni mwa Wayahudi waliokwisha pokea imani, hawa tu peke yao, ndio wanaofanya kazi pamoja nami kwa ajili ya ufalme wa Mungu; nao wamekuwa msaada mkubwa kwangu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Naye Yesu anayeitwa Yusto anawasalimu. Kwao Wakristo wa Kiyuda ni hao watatu tu walio wenzangu wa kazi ya kuujenga ufalme wa Mungu, ndio walionituliza moyo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na Yesu aitwaye Yusto; hao ni watu wa tohara. Tena hao peke yao ni watendaji wa kazi pamoja nami kwa ajili ya ufalme wa Mungu; nao walikuwa faraja kwangu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Naye Yesu anayeitwa Yusto, anawasalimia ninyi vilevile. Kati ya Wayuda walioamini ni hao watatu tu ndio wanaotumika pamoja nami kwa ajili ya kazi inayoelekea Ufalme wa Mungu, nao wamenifariji sana.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Na Yesu aitwae Yusto; hao ni watu wa tohara. Tena hao peke yao ni watendaji wa kazi pamoja nami kwa ajili ya ufalme wa Mungu; nao walikuwa faraja kwangu.