Colossians 4:12 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Epafra, mwananchi mwenzenu na mtumishi wa Kristo Yesu, anawasalimuni. Daima anawaombeeni nyinyi kwa bidii ili mpate kusimama imara, mkomae na kuwa thabiti kabisa katika mambo yote anayotaka Mungu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Epafra, ambaye ni mmoja wenu na mtumishi wa Al-Masihi Isa, anawasalimu. Yeye siku zote anawaombea kwa bidii kwamba msimame imara katika mapenzi yote ya Mungu, mkiwa wakamilifu na thabiti.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Epafra, aliye mtu wa kwenu, mtumwa wa Yesu Kristo, awasalimu, akifanya bidii siku zote kwa ajili yenu katika maombi yake, ili kwamba msimame wakamilifu na kuthibitika sana katika mapenzi yote ya Mungu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Epafra, mtumishi mwingine wa Yesu Kristo, kutoka kwenu anawasalimu. Yeye anahangaika kwa ajili yenu kwa kuwaombea mara kwa mara, ili mkue kiroho na kupokea kila kitu ambacho Mungu anataka kwa ajili yangu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Epafra, mwananchi mwenzenu na mtumishi wa Kristo Yesu anawasalimuni. Daima anawaombeeni ninyi kwa bidii ili mpate kusimama imara, mkomae na kuwa thabiti kabisa katika mambo yote anayotaka Mungu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Epafra, mwananchi mwenzenu na mtumishi wa Kristo Yesu, anawasalimuni. Daima anawaombeeni nyinyi kwa bidii ili mpate kusimama imara, mkomae na kuwa thabiti kabisa katika mambo yote anayotaka Mungu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Epafra, ambaye ni mmoja wenu na mtumishi wa Kristo Yesu, anawasalimu. Yeye siku zote anawaombea kwa bidii kwamba msimame imara katika mapenzi yote ya Mungu mkiwa wakamilifu na thabiti.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Epafra, ambaye ni mmoja wenu na mtumishi wa Al-Masihi Isa, anawasalimu. Yeye siku zote anawaombea kwa bidii kwamba msimame imara katika mapenzi yote ya Mwenyezi Mungu, mkiwa wakamilifu na thabiti.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Epafra, aliye mtu wa kwenu, mtumwa wa Yesu Kristo, awasalimu, akifanya bidii siku zote kwa ajili yenu katika maombi yake, ili msimame mkiwa wakamilifu na kuthibitika kabisa katika mapenzi yote ya Mungu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Epafra, mwananchi mwenzenu na mtumishi wa Kristo Yesu, anawasalimuni. Daima anawaombeeni nyinyi kwa bidii ili mpate kusimama imara, mkomae na kuwa thabiti kabisa katika mambo yote anayotaka Mungu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Epafura aliye wa kwenu anawasalimu; ni mtumwa wa Kristo Yesu, naye huwagombea kila siku na kuwaombea, mpate kusimama wenye kuyatimiza na kuyatambua yote, Mungu ayatakayo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Epafra, aliye mtu wa kwenu, mtumwa wa Yesu Kristo, awasalimu, akifanya bidii siku zote kwa ajili yenu katika maombi yake, ili kwamba msimame wakamilifu na kuthibitika sana katika mapenzi yote ya Mungu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mwanainchi mwenzenu Epafra anawasalimia vilevile. Yeye ni mutumishi wa Yesu Kristo, hachoki kwa kuwaombea ninyi, kusudi musimame imara mukikomaa kiroho na kuwa tayari kwa kutimiza kabisa mapenzi ya Mungu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Epafra, aliye mtu wa kwenu, mtumwa wa Yesu Kristo, awasalimu, akifanya bidii siku zote kwa ajili yenu, katika maombi yake msimame wakamilifu mkathuhutike sana katika mapenzi yote ya Mungu.