Colossians 4:15 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Salamu zetu kwa ndugu wa Laodikea. Msalimuni dada Nimfa pamoja na jumuiya yote ya waumini inayokutana nyumbani kwake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wasalimuni ndugu wote wa Laodikia, na pia Nimfa, pamoja na kundi la waumini wanaokutana katika nyumba yake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wasalimuni ndugu walioko Laodikia, na Nimfa, na kanisa lililo katika nyumba yake.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Wasalimuni kaka na dada zetu walioko Laodikia. Msalimuni pia Nimfa na kanisa lililo katika nyumba yake.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Salamu zetu kwa ndugu zetu wa Laodikea; msalimuni dada Nimfa pamoja na jumuiya yote ya waumini inayokutana nyumbani kwake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Salamu zetu kwa ndugu wa Laodikea. Msalimuni dada Nimfa pamoja na jumuiya yote ya waumini inayokutana nyumbani kwake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wasalimuni ndugu wote wa Laodikia na pia Nimfa pamoja na kanisa linalokutana katika nyumba yake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wasalimuni ndugu wote wa Laodikia, na pia Nimfa, pamoja na kundi la waumini linalokutana katika nyumba yake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wasalimuni ndugu walioko Laodikia, na Nimfa, na kanisa lililo katika nyumba yake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Salamu zetu kwa ndugu wa Laodikea. Msalimuni dada Nimfa pamoja na jumuiya yote ya waumini inayokutana nyumbani kwake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wasalimieni ndugu walioko Laodikia, naye Nimfa nao wateule waliomo nyumbani mwake!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wasalimuni ndugu walioko Laodikia, na Nimfa, na kanisa lililo katika nyumba yake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Muwasalimie wandugu wa Laodikia, pamoja na Nimfa na kanisa linalokusanyika ndani ya nyumba yake.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Wasalimuni ndugu walio katika Laodikia, na Numfa, na kanisa lililo katika nyumba yake.