Colossians 4:16 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mkisha soma barua hii, hakikisheni kwamba inasomwa na Wakristo wa Laodikea; na nyinyi fanyeni mpango mpate kuisoma barua waliyoipata wao.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Baada ya barua hii kusomwa kwenu, hakikisheni kwamba inasomwa pia katika kundi la waumini wa Walaodikia. Nanyi pia msome barua inayotoka Laodikia.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Waraka huu ukiisha kusomwa kwenu fanyeni kwamba usomwe katika kanisa la Walaodikia pia; na ule wa Laodikia usomwe na ninyi.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Baada ya kusoma barua hii, ipelekeni katika kanisa la Laodikia, ili isomwe huko pia. Ninyi nanyi msome barua niliyowaandikia wao.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Mkisha soma barua hii, hakikisheni kwamba inasomwa na Wakristo wa Laodikea; na ninyi fanyeni mpango mpate kuisoma barua waliyoipata kwao.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mkisha soma barua hii, hakikisheni kwamba inasomwa na Wakristo wa Laodikea; na nyinyi fanyeni mpango mpate kuisoma barua waliyoipata wao.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Baada ya barua hii kusomwa kwenu, hakikisheni kwamba inasomwa pia katika kanisa la Walaodikia. Nanyi pia msome barua inayotoka Laodikia.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Baada ya barua hii kusomwa kwenu, hakikisheni kwamba inasomwa pia katika kundi la waumini la Walaodikia. Nanyi pia msome barua inayotoka Laodikia.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Waraka huu ukiisha kusomwa kwenu hakikisheni kwamba unasomwa katika kanisa la Walaodikia pia; na ule wa Laodikia usomwe na ninyi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mkisha soma barua hii, hakikisheni kwamba inasomwa na Wakristo wa Laodikea; na nyinyi fanyeni mpango mpate kuisoma barua waliyoipata wao.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Barua hii, ikiisha kusomwa kwenu, angalieni, isomwe hata kwao wateule wa Laodikia, nanyi mwisome ile ya Laodikia!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Waraka huu ukiisha kusomwa kwenu fanyeni kwamba usomwe katika kanisa la Walaodikia pia; na ule wa Laodikia usomwe na ninyi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Barua hii itakapokwisha kusomwa kwenu mufanye namna yote ipate kusomwa vilevile katika kanisa la Laodikia. Na ninyi kwa ngambo yenu, musome vilevile barua niliyotuma kwa kanisa lile.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Waraka hun ukiisha kusomwa kwenu, fanyeni kwamba usomwe katika kanisa la Walaodikia; na ule wa Laodikia usomwe na ninyi.