Colossians 4:18 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Naandika haya kwa mkono wangu mwenyewe: Salamu kutoka kwangu, mimi Paulo. Kumbukeni kwamba niko kifungoni. Neema ya Mungu iwe nanyi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mimi Paulo naandika salamu hizi kwa mkono wangu mwenyewe. Kumbukeni minyororo yangu. Neema iwe nanyi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Salamu yangu mimi Paulo, kwa mkono wangu mwenyewe. Kumbukeni kufungwa kwangu. Neema na iwe pamoja nanyi.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Hii ni salamu yangu ambayo nimeiandika kwa mkono wangu mwenyewe: PAULO. Msiache kunikumbuka nikiwa hapa gerezani. Ninawaombea neema ya Mungu iwe pamoja nanyi nyote.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Naandika haya kwa mkono wangu mwenyewe: Salamu kutoka kwangu, mimi Paulo. Kumbukeni kwamba niko kifungoni. Neema ya Mungu iwe nanyi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Naandika haya kwa mkono wangu mwenyewe: Salamu kutoka kwangu, mimi Paulo. Kumbukeni kwamba niko kifungoni. Neema ya Mungu iwe nanyi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mimi, Paulo, naandika salamu hizi kwa mkono wangu mwenyewe. Kumbukeni minyororo yangu. Neema iwe nanyi. Amen.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mimi, Paulo, naandika salamu hizi kwa mkono wangu mwenyewe. Kumbukeni minyororo yangu. Neema iwe nanyi. Amen.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Naandika salamu yangu mimi Paulo, kwa mkono wangu mwenyewe. Kumbukeni kufungwa kwangu. Neema na iwe pamoja nanyi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Naandika haya kwa mkono wangu mwenyewe: Salamu kutoka kwangu, mimi Paulo. Kumbukeni kwamba niko kifungoni. Neema ya Mungu iwe nanyi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Salamu hii naiandika kwa mkono wangu mimi Paulo. Ikumbukeni hii minyororo yangu! Upole uwakalie! Amin.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Salamu yangu mimi Paulo, kwa mkono wangu mwenyewe. Kumbukeni kufungwa kwangu. Neema na iwe pamoja nanyi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mimi Paulo ninawatumia salamu zangu, nikiziandika kwa mukono wangu mwenyewe. Musisahau kwamba mimi ningali katika kifungo. Ninawatakia neema kutoka kwa Mungu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Salamu yangu mimi Paolo, kwa mkono wangu mwenyewe. Yakumbukeni mafungo yangu. Neema na iwe pamoja nanyi. Amin.