Colossians 4:3 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Vilevile, mtuombee sisi pia ili Mungu atupe fursa ya kuuhubiri ujumbe wake kuhusu siri ya Kristo. Kwa ajili hiyo mimi niko sasa kifungoni.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Pia tuombeeni na sisi ili Mungu atufungulie mlango wa kunena neno lake, ili tupate kuitangaza siri ya Al-Masihi, ambayo kwa ajili yake nimefungwa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
mkituombea na sisi pia, kwamba Mungu atufungulie mlango kwa lile neno lake, tuinene siri ya Kristo, ambayo kwa ajili yake nimefungwa,
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Mtuombee na sisi pia, ili Mungu atupe fursa za kuwaeleza watu ujumbe wake. Nimefungwa kwa sababu ya hili. Lakini ombeni ili tuendelee kuwaeleza watu siri ya kweli ambayo Mungu ameiweka wazi kuhusu Kristo.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Vilevile, mtuombee sisi pia ili Mungu atupe fursa ya kuuhubiri ujumbe wake kuhusu siri ya Kristo. Kwa ajili hiyo mimi niko sasa kifungoni.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Vilevile, mtuombee sisi pia ili Mungu atupe fursa ya kuuhubiri ujumbe wake kuhusu siri ya Kristo. Kwa ajili hiyo mimi niko sasa kifungoni.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Pia tuombeeni na sisi ili Mungu atufungulie mlango wa kunena, ili tupate kuitangaza siri ya Kristo, ambayo kwa ajili yake pia mimi nimefungwa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Pia tuombeeni na sisi ili Mwenyezi Mungu atufungulie mlango wa kunena, ili tupate kuitangaza siri ya Al-Masihi, ambayo kwa ajili yake pia mimi nimefungwa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
mkituombea na sisi pia, kwamba Mungu atufungulie mlango kwa lile neno lake, tuinene siri ya Kristo, ambayo kwa ajili yake nimefungwa,
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Vilevile, mtuombee sisi pia ili Mungu atupe fursa ya kuuhubiri ujumbe wake kuhusu siri ya Kristo. Kwa ajili hiyo mimi niko sasa kifungoni.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Na sisi vilevile tuombeeni, Mungu atufungulie mlango wa kuingizamo Neno lake, tupate kulisema fumbo la Kristo, ni lilelile, nililofungiwa,
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
mkituombea na sisi pia, kwamba Mungu atufungulie mlango kwa lile neno lake, tuinene siri ya Kristo, ambayo kwa ajili yake nimefungwa,
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mutuombee sisi vilevile kusudi Mungu atufungulie njia ya kuhubiri neno lake tupate kutangaza ujumbe wa siri juu ya Kristo. Ni kwa ajili ya ujumbe ule mimi niko sasa katika kifungo.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
mkituombea na sisi pia, Mungu atufungulie mlango kwa Neno lake tuinene siri ya Kristo, ambayo kwa ajili yake nimefungwa,