Colossians 4:6 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mazungumzo yenu yanapaswa kuwa daima mema na yaliyokolezwa kwa chumvi na ya kuvutia, na mnapaswa kujua jinsi ya kumjibu vizuri kila mmoja.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Maneno yenu yawe yamejaa neema siku zote, yanayofaa, ili mjue jinsi iwapasavyo kumjibu kila mtu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Maneno yenu yawe na neema siku zote, yakikolea munyu, mpate kujua jinsi iwapasavyo kumjibu kila mtu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kila mnapozungumza pamoja na walio nje ya kundi lenu, muwe wema na wenye hekima. Ndipo mtaweza kumjibu kila mtu ipasavyo.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Mazungumzo yenu yanapaswa kuwa daima mema na ya kuvutia, na mnapaswa kujua jinsi ya kumjibu vizuri kila mmoja.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mazungumzo yenu yanapaswa kuwa daima mema na yaliyokolezwa kwa chumvi na ya kuvutia, na mnapaswa kujua jinsi ya kumjibu vizuri kila mmoja.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Maneno yenu yawe yamejaa neema siku zote, yanayofaa, ili mjue jinsi iwapasavyo na inavyofaa kumjibu kila mtu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Maneno yenu yawe yamejaa neema siku zote, yanayofaa, ili mjue jinsi iwapasavyo na inavyofaa kumjibu kila mtu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Maneno yenu yawe na neema siku zote, yakikolezwa chumvi, ili mpate kujua jinsi iwapasavyo kumjibu kila mtu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mazungumzo yenu yanapaswa kuwa daima mema na yaliyokolezwa kwa chumvi na ya kuvutia, na mnapaswa kujua jinsi ya kumjibu vizuri kila mmoja.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Maneno yenu yawe po pote ya kupendeza yakiwa matamu kama yenye chumvi, mpate kujua yanayofaa ya kumjibu mtu awaye yote!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Maneno yenu yawe na neema siku zote, yakikolea munyu, mpate kujua jinsi iwapasavyo kumjibu kila mtu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Masemi yenu yanapaswa kuwa mazuri siku zote na yenye kufaa, munapaswa kujua kujibia kila mutu vizuri.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Maneno yenu yawe na neema siku zote, yakikolea chumvi, mpate kujua jinsi iwapasa vyo kumjibu killa mtu.