Daniel 1:10 — Compare Translations
9 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini, towashi mkuu akamwambia Danieli, “Nina hofu kwamba bwana wangu mfalme ambaye ametoa maagizo kuhusu chakula na vinywaji unavyopaswa kutumia, ataona kuwa afya yako si nzuri kama ya wenzako wa rika lako. Hivyo maisha yangu yatakuwa hatarini.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini huyo mkuu wa maafisa akamwambia Danieli, “Ninamwogopa bwana wangu mfalme, aliyeagizia chakula na kinywaji chenu. Kwa nini aone nyuso zenu zikiwa mbaya kuliko za vijana wengine wa rika lenu? Mfalme atakata kichwa changu kwa sababu yenu.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mkuu wa matowashi akamwambia Danieli, Mimi namwogopa bwana wangu, mfalme, aliyewaagizia ninyi chakula chenu na kinywaji chenu; kwa nini azione nyuso zenu kuwa hazipendezi kama nyuso za vijana hirimu zenu? Basi kwa kufanya hivyo mtahatirisha kichwa changu mbele ya mfalme.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini, towashi mkuu akamwambia Danieli, “Nina hofu kwamba bwana wangu mfalme ambaye ametoa maagizo kuhusu chakula na vinywaji unavyopaswa kutumia, ataona kuwa afya yako si nzuri kama ya wenzako wa rika lako. Hivyo maisha yangu yatakuwa hatarini.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
lakini huyo mkuu wa maafisa akamwambia Danieli, “Ninamwogopa bwana wangu mfalme, aliyeagizia chakula na kinywaji chenu. Kwa nini aone nyuso zenu ni mbaya kuliko za vijana rika lenu? Mfalme atakata kichwa changu kwa sababu yenu.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
lakini huyo mkuu wa maafisa akamwambia Danieli, “Ninamwogopa bwana wangu mfalme, aliyeagizia chakula na kinywaji chenu. Kwa nini aone nyuso zenu zikiwa mbaya kuliko za vijana wengine wa rika lenu? Mfalme atakata kichwa changu kwa sababu yenu.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Naye mkuu wa watumishi wa nyumbani akamjibu Danieli: Mimi ninamwogopa bwana wangu mfalme, aniagiziaye vilaji na vinywaji vyenu; kama angewaona ninyi, ya kuwa nyuso zenu zinanuna kuliko zao vijana wengine walio rika moja nanyi, basi, mtakuwa mmeniponza kwake mfalme, akanikata kichwa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mkuu wa matowashi akamwambia Danieli, Mimi namwogopa bwana wangu, mfalme, aliyewaagizia ninyi chakula chenu na kinywaji chenu; kwa nini azione nyuso zenu kuwa hazipendezi kama nyuso za vijana hirimu zenu? Basi kwa kufanya hivyo mtahatirisha kichwa changu mbele ya mfalme.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini, mukubwa yule akamwambia Danieli: Ninaogopa kwamba bwana wangu mufalme ambaye ametoa maagizo juu ya chakula na kinywaji unavyopaswa kutumia, ataona kwamba afya yako si nzuri kama ya wenzako wa umri wako. Hivyo maisha yangu yatakuwa katika hatari.