Daniel 1:13 — Compare Translations

9 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha, tulinganishe sisi na hao vijana wengine wanaokula chakula cha mfalme, halafu utoe uamuzi wako kulingana na jinsi utakavyoona.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Baadaye ulinganishe sura zetu na vijana wanaokula chakula cha mfalme, ukawatendee watumishi wako kulingana na unachoona.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kisha nyuso zetu zitazamwe mbele yako, na nyuso za wale vijana wanaokula chakula cha mfalme; ukatutendee sisi watumishi wako kadiri ya utakavyoona.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha, tulinganishe sisi na hao vijana wengine wanaokula chakula cha mfalme, halafu utoe uamuzi wako kulingana na jinsi utakavyoona.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ndipo ulinganishe kuonekana kwetu na vijana wanaokula chakula cha kifalme, ukawatendee watumishi wako kulingana na unachoona.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Baadaye ulinganishe sura zetu na vijana wanaokula chakula cha mfalme, ukawatendee watumishi wako kulingana na unachoona.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha tutazamwe mbele yako, tulivyo, nao vijana wanaokula vilaji vya urembo vya mfalme watazamwe nao, walivyo. Kama utakavyoona, basi, ndivyo, utakavyotufanyizia sisi watumwa wako.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kisha nyuso zetu zitazamwe mbele yako, na nyuso za wale vijana wanaokula chakula cha mfalme; ukatutendee sisi watumishi wako kadiri ya utakavyoona.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha, utulinganishe sisi na hao vijana wengine wanaokula chakula cha mufalme, halafu utoe uamuzi wako kulingana na jinsi utakavyoona.