Daniel 1:15 — Compare Translations

9 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Baada ya siku hizo kumi, aliwaangalia akaona kuwa wale vijana waliokula mboga za majani walionekana wenye afya na nguvu kuliko wale wengine wote waliolishwa chakula cha kifalme.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mwisho wa zile siku kumi, walionekana kuwa na afya na kunawiri kuliko yeyote kati ya vijana waliokula chakula cha mfalme.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hata mwisho wa zile siku kumi nyuso zao zilikuwa nzuri zaidi, na miili yao ilikuwa imenenepa zaidi, kuliko wale vijana wote waliokula chakula cha mfalme.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Baada ya siku hizo kumi, aliwaangalia akaona kuwa wale vijana waliokula mboga za majani walionekana wenye afya na nguvu kuliko wale wengine wote waliolishwa chakula cha kifalme.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mwisho wa zile siku kumi walionekana kuwa na afya na kunawiri zaidi kuliko ye yote kati ya wale vijana waliokula chakula cha kifalme.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mwisho wa zile siku kumi, walionekana kuwa na afya na kunawiri zaidi kuliko yeyote kati ya wale vijana waliokula chakula cha mfalme.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Siku kumi zilipokwisha pita, wakatazamwa, wakaonekana kuwa wema, nayo miili yao ilikuwa imenona kuliko vijana wote waliovila vilaji vya urembo vya mfalme.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hata mwisho wa zile siku kumi nyuso zao zilikuwa nzuri zaidi, na miili yao ilikuwa imenenepa zaidi, kuliko wale vijana wote waliokula chakula cha mfalme.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha siku hizo kumi, aliwaangalia akaona kwamba wale vijana waliokula mboga za majani walionekana wenye afya na nguvu kuliko wale wengine wote waliokulishwa chakula cha kifalme.