Daniel 1:17 — Compare Translations

9 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mungu aliwajalia vijana hao wanne maarifa na ujuzi katika elimu na hekima. Zaidi ya hayo, alimjalia Danieli kipawa cha kufasiri maono na ndoto.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mungu akawapa hawa vijana wanne maarifa na ufahamu wa kila aina ya maandiko na elimu. Naye Danieli aliweza kufahamu maono na aina zote za ndoto.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi, kwa habari za hao vijana wanne, Mungu aliwapa maarifa na ujuzi katika elimu na hekima; Danieli naye alikuwa na ufahamu katika maono yote, na ndoto.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mungu aliwajalia vijana hao wanne maarifa na ujuzi katika elimu na hekima. Zaidi ya hayo, alimjalia Danieli kipawa cha kufasiri maono na ndoto.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mungu akawapa hawa vijana waume wanne maarifa na ufahamu wa kila aina ya maandiko na elimu. Naye Danieli aliweza kufahamu maono na aina zote za ndoto.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mungu akawapa hawa vijana wanne maarifa na ufahamu wa kila aina ya maandiko na elimu. Naye Danieli aliweza kufahamu maono na aina zote za ndoto.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Naye Mungu akawapa hawa vijana wanne akili za kujifunza ujuzi wote uliokuwamo katika vitabu, naye Danieli akampa kutambua maono na ndoto zote.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi, kwa habari za hao vijana wanne, Mungu aliwapa maarifa na ujuzi katika elimu na hekima; Danieli naye alikuwa na ufahamu katika maono yote, na ndoto.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mungu aliwajalia vijana wale wane maarifa na ujuzi katika elimu na hekima. Zaidi ya hayo, alimujalia Danieli ufahamu wa kufasiria maono na ndoto.