Daniel 1:19 — Compare Translations

9 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mfalme alipozungumza nao wote, hakuna walioonekana kuwa bora kama Danieli, Hanania, Mishaeli na Azaria. Basi, wakakubaliwa kumhudumia mfalme.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mfalme akazungumza nao, akaona hakuna aliyelingana na Danieli, Hanania, Mishaeli na Azaria. Hivyo wakaingia katika utumishi wa mfalme.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naye mfalme akazungumza nao; na miongoni mwao wote hawakuonekana waliokuwa kama Danieli, na Hanania, na Mishaeli, na Azaria; kwa hiyo wakasimama mbele ya mfalme.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mfalme alipozungumza nao wote, hakuna walioonekana kuwa bora kama Danieli, Hanania, Mishaeli na Azaria. Basi, wakakubaliwa kumhudumia mfalme.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mfalme akazungumza nao, akaona hakuna aliyekuwa amelingana na Danieli, Hanania, Mishaeli na Azaria, hivyo wakaingia katika utumishi wa mfalme.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mfalme akazungumza nao, akaona hakuna aliyelingana na Danieli, Hanania, Mishaeli na Azaria. Hivyo wakaingia katika utumishi wa mfalme.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mfalme alipoongea nao, kwao wote hakuoneka aliyefanana nao akina Daniel na Hanania na Misaeli na Azaria; kwa hiyo wakapewa kumtumikia mfalme.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naye mfalme akazungumza nao; na miongoni mwao wote hawakuonekana waliokuwa kama Danieli, na Hanania, na Mishaeli, na Azaria; kwa hiyo wakasimama mbele ya mfalme.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mufalme alipozungumuza nao wote, hakuna walioonekana kuwa bora kama Danieli, Hanania, Misaeli na Azaria. Basi, wakakubaliwa kumutumikia mufalme.