Daniel 1:2 — Compare Translations

9 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Bwana akamwacha Yehoyakimu atiwe mikononi mwa mfalme Nebukadneza pamoja na baadhi ya vyombo vya nyumba ya Mungu. Basi mfalme Nebukadneza akachukua mateka na vyombo akavipeleka nchini Shinari, akaviweka katika hazina ya miungu yake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Bwana akamtia Yehoyakimu mfalme wa Yuda mkononi mwa Nebukadneza, pamoja na baadhi ya vyombo kutoka Hekalu la Mungu. Nebukadneza akavichukua hadi kwenye hekalu la mungu wake huko Shinari, naye akaviweka nyumbani ya hazina ya mungu wake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Bwana akamtia Yehoyakimu, mfalme wa Yuda, katika mkono wake, pamoja na baadhi ya vyombo vya nyumba ya Mungu; naye akavichukua mpaka nchi ya Shinari, mpaka nyumba ya mungu wake; akaviingiza vile vyombo katika nyumba ya hazina ya mungu wake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Bwana akamwacha Yehoyakimu atiwe mikononi mwa mfalme Nebukadneza pamoja na baadhi ya vyombo vya nyumba ya Mungu. Basi mfalme Nebukadneza akachukua mateka na vyombo akavipeleka nchini Shinari, akaviweka katika hazina ya miungu yake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Bwana akamtia Yehoyakimu mfalme wa Yuda mkononi mwa Nebukadneza pamoja na baadhi ya vyombo kutoka katika Hekalu la Mungu. Hivi akavichukua hadi kwenye hekalu la mungu wake huko Shinari naye akaviweka katika nyumba ya hazina ya mungu wake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Bwana akamtia Yehoyakimu mfalme wa Yuda mkononi mwa Nebukadneza, pamoja na baadhi ya vyombo kutoka Hekalu la Mungu. Hivi akavichukua hadi kwenye hekalu la mungu wake huko Shinari, naye akaviweka nyumbani ya hazina ya mungu wake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Bwana akamtia Yoyakimu, mfalme wa Yuda, mkononi mwake, hata vyombo vinginevyo vya Nyumbani mwa Mungu akavipeleka katika nchi ya Sinari nyumbani mwa miungu yake, kisha akavipeleka hivyo vyombo katika nyumba ya vilimbiko vya miungu yake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Bwana akamtia Yehoyakimu, mfalme wa Yuda, katika mkono wake, pamoja na baadhi ya vyombo vya nyumba ya Mungu; naye akavichukua mpaka nchi ya Shinari, mpaka nyumba ya mungu wake; akaviingiza vile vyombo katika nyumba ya hazina ya mungu wake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Bwana akamwacha Yoyakimu atiwe katika mikono ya mufalme Nebukadneza pamoja na sehemu ya vyombo vya nyumba ya Mungu. Basi mufalme Nebukadneza akakamata wafungwa na vyombo akavipeleka katika inchi ya Babeli, akaviweka katika hazina ya nyumba ya miungu yake.