Daniel 1:3 — Compare Translations
9 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mfalme Nebukadneza akamwamuru Ashpenazi, towashi wake mkuu, amchagulie baadhi ya vijana wa Israeli wa jamaa ya kifalme na ya watu mashuhuri.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kisha mfalme akamwagiza Ashpenazi, mkuu wa maafisa wa mfalme, kumletea baadhi ya Waisraeli kutoka jamaa ya mfalme na kutoka jamaa kuu:
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mfalme akamwambia Ashpenazi, mkuu wa matowashi wake, awalete baadhi ya wana wa Israeli, wa uzao wa kifalme, na wa uzao wa kiungwana;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mfalme Nebukadneza akamwamuru Ashpenazi, towashi wake mkuu, amchagulie baadhi ya vijana wa Israeli wa jamaa ya kifalme na ya watu mashuhuri.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kisha mfalme akamwagiza Ashpenazi, mkuu wa maafisa wa jumba lake la kifalme, kumletea baadhi ya Waisraeli kutoka jamaa ya kifalme na kutoka watu mashuhuri,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kisha mfalme akamwagiza Ashpenazi, mkuu wa maafisa wa mfalme, kumletea baadhi ya Waisraeli kutoka jamaa ya mfalme na kutoka jamaa kuu,
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mfalme akamwambia Asipenazi aliyekuwa mkuu wa watumishi wake wa nyumbani, alete wana wa Kiisiraeli walio wa uzao wa kifalme na wa watu wenye macheo;
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mfalme akamwambia Ashpenazi, mkuu wa matowashi wake, awalete baadhi ya wana wa Israeli, wa uzao wa kifalme, na wa uzao wa kiungwana;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mufalme Nebukadneza akamwamuru Aspenazi, mukubwa wa watumishi wake, amuchagulie kati ya vijana wa Waisraeli wa jamaa ya kifalme na ya watu wenye heshima.