Daniel 1:4 — Compare Translations
9 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mfalme alitaka vijana wasio na kasoro, wazuri kwa umbo, wenye uzoefu wa kila hekima, wenye akili na maarifa na wanaofaa kutoa huduma katika ikulu. Alitaka pia vijana hao wafundishwe kusoma na kuandika lugha ya Wakaldayo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
vijana wa kiume wasio na dosari mwilini, wenye sura nzuri, wanaoonesha kipaji katika kila aina ya elimu, wenye ufahamu mzuri, wepesi kuelewa, na waliofuzu kuhudumu katika jumba la kifalme. Alikuwa awafundishe lugha na maandiko ya Wakaldayo.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
vijana wasio na mawaa, wazuri wa uso, wajuzi wa hekima, werevu kwa sababu ya maarifa yao, wenye kufahamu elimu, watakaoweza kusimama katika jumba la mfalme; tena alimwambia awafundishe elimu ya Wakaldayo, na lugha yao.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mfalme alitaka vijana wasio na kasoro, wazuri kwa umbo, wenye uzoefu wa kila hekima, wenye akili na maarifa na wanaofaa kutoa huduma katika ikulu. Alitaka pia vijana hao wafundishwe kusoma na kuandika lugha ya Wakaldayo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
vijana wanaume wasio na dosari mwilini, wenye sura nzuri, wanaoonyesha ujuzi katika kila elimu, wenye ufahamu mzuri, wepesi kuelewa, na waliofuzu kuhudumu katika jumba la kifalme. Alikuwa awafundishe lugha na maandiko ya Wakaldayo.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
vijana wanaume wasio na dosari mwilini, wenye sura nzuri, wanaoonyesha kipaji katika kila aina ya elimu, wenye ufahamu mzuri, wepesi kuelewa, na waliofuzu kuhudumu katika jumba la kifalme. Alikuwa awafundishe lugha na maandiko ya Wakaldayo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
achague wavulana wasio na kilema cho chote, wenye miili mizuri ya kupendeza, wenye ubingwa na ujuzi wote, wenye akili za kujua na za kutambua wanayoelezwa, wenye nguvu za kutumikia jumbani mwa mfalme, apate kuwafundisha maandiko na maneno ya Wakasidi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
vijana wasio na mawaa, wazuri wa uso, wajuzi wa hekima, werevu kwa sababu ya maarifa yao, wenye kufahamu elimu, watakaoweza kusimama katika jumba la mfalme; tena alimwambia awafundishe elimu ya Wakaldayo, na lugha yao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mufalme alitaka vijana wasiokuwa na kilema, wazuri kwa umbo, wenye ujuzi wa kila hekima, wenye akili na maarifa na wanaofaa kwa kutumika katika nyumba ya kifalme. Alitaka vilevile vijana wale wafundishwe kusoma na kuandika luga ya Wakaldea.