Daniel 1:5 — Compare Translations

9 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mfalme aliagiza vijana hao wapewe chakula bora ambacho yeye mwenyewe alikula na divai ambayo alikunywa. Vijana hao walitakiwa wapewe mafunzo kwa miaka mitatu, kisha wapelekwe kwa mfalme.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mfalme akawaagizia kiasi cha chakula na divai ya kila siku kutoka meza ya mfalme. Walikuwa wafundishwe kwa miaka mitatu, na hatimaye waingie kwenye utumishi wa mfalme.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Huyo mfalme akawaagizia posho ya chakula cha mfalme, na ya divai aliyokunywa, akaagiza walishwe hivyo muda wa miaka mitatu; ili kwamba hatimaye wasimame mbele ya mfalme.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mfalme aliagiza vijana hao wapewe chakula bora ambacho yeye mwenyewe alikula na divai ambayo alikunywa. Vijana hao walitakiwa wapewe mafunzo kwa miaka mitatu, kisha wapelekwe kwa mfalme.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mfalme akawaagizia kiasi cha chakula na divai ya kila siku kutoka katika meza ya mfalme. Walikuwa wafundishwe kwa miaka mitatu, hatimaye waingie kwenye utumishi wa mfalme.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mfalme akawaagizia kiasi cha chakula na divai ya kila siku kutoka meza ya mfalme. Walikuwa wafundishwe kwa miaka mitatu, na hatimaye waingie kwenye utumishi wa mfalme.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mfalme akawaagizia siku ya siku vilaji vya urembo, yeye mfalme alivyovila, hata mvinyo, alizozinywa; akataka, wafugwe hivyo miaka mitatu, kisha wamtumikie mfalme.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Huyo mfalme akawaagizia posho ya chakula cha mfalme, na ya divai aliyokunywa, akaagiza walishwe hivyo muda wa miaka mitatu; ili kwamba hatimaye wasimame mbele ya mfalme.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mufalme aliagiza vijana wale wapewe chakula bora ambacho yeye mwenyewe alikula na divai ambayo alikunywa. Aliagiza vilevile vijana wale wafundishwe kwa miaka mitatu, kisha wapelekwe kwa mufalme.