Daniel 1:7 — Compare Translations
9 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Huyo towashi mkuu akawapa majina mengine; Danieli akamwita Belteshaza, Hanania akamwita Shadraki, Mishaeli akamwita Meshaki na Azaria akamwita Abednego.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mkuu wa maafisa akawapa majina mapya: Danieli akamwita jina Belteshaza, Hanania akamwita jina Shadraki, Mishaeli akamwita jina Meshaki, na Azaria akamwita jina Abednego.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mkuu wa matowashi akawapa majina; alimwita Danieli, Belteshaza; na Hanania akamwita Shadraka; na Mishaeli akamwita Meshaki; na Azaria akamwita Abednego.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Huyo towashi mkuu akawapa majina mengine; Danieli akamwita Belteshaza, Hanania akamwita Shadraki, Mishaeli akamwita Meshaki na Azaria akamwita Abednego.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mkuu wa maafisa akawapa majina mapya, Danieli akamwita Belteshaza, Hanania akamwita Shadraki, Mishaeli akamwita Meshaki na Azaria akamwita Abednego.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mkuu wa maafisa akawapa majina mapya: Danieli akamwita Belteshaza, Hanania akamwita Shadraki, Mishaeli akamwita Meshaki, na Azaria akamwita Abednego.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Naye mkuu wa watumishi wa nyumbani akawapa majina mengine: Danieli akamwita Beltesasari, naye Hanania akamwita Sadiraki, naye Misaeli akamwita Mesaki, naye Azaria akamwita Abedi-Nego.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mkuu wa matowashi akawapa majina; alimwita Danieli, Belteshaza; na Hanania akamwita Shadraka; na Mishaeli akamwita Meshaki; na Azaria akamwita Abednego.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yule mukubwa wa watumishi akawapa majina mengine; akamwita Danieli kwa jina la Beltesaza, Hanania kwa jina la Sadiraki, Misaeli kwa jina la Mesaki na Azaria kwa jina la Abedenego.