Daniel 1:8 — Compare Translations
9 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini Danieli aliamua kutojitia unajisi kwa kula chakula bora cha mfalme na kunywa divai yake. Kwa hiyo, alimwomba towashi mkuu amruhusu asile vitu hivyo na kujitia unajisi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini Danieli alikusudia kuwa hatajinajisi kwa chakula cha mfalme na divai, naye akamwomba mkuu wa maafisa ruhusa ili asijinajisi kwa njia hii.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini Danieli aliazimu moyoni mwake ya kuwa hatajitia unajisi kwa chakula cha mfalme, wala kwa divai aliyokunywa; basi akamwomba yule mkuu wa matowashi ampe ruhusa asijitie unajisi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini Danieli aliamua kutojitia unajisi kwa kula chakula bora cha mfalme na kunywa divai yake. Kwa hiyo, alimwomba towashi mkuu amruhusu asile vitu hivyo na kujitia unajisi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini Danieli alikusudia kuwa hatajitia unajisi kwa chakula cha kifalme na divai, naye akamwomba mkuu wa maafisa ruhusa kwa ajili ya kutokujinajisi kwa njia hii.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini Danieli alikusudia kuwa hatajitia unajisi kwa chakula cha mfalme na divai, naye akamwomba mkuu wa maafisa ruhusa ili asijinajisi kwa njia hii.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini Danieli alisema moyoni mwake: Sitajipatia uchafu nikila vilaji vya urembo vya mfalme au nikinywa mvinyo zake; akamwomba mkuu wa watumishi wa nyumbani ruhusa, asijipatie uchafu hivyo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini Danieli aliazimu moyoni mwake ya kuwa hatajitia unajisi kwa chakula cha mfalme, wala kwa divai aliyokunywa; basi akamwomba yule mkuu wa matowashi ampe ruhusa asijitie unajisi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini Danieli aliamua kutojichafua kwa kula chakula bora cha mufalme na kunywa divai yake. Kwa hiyo, alimwomba yule mukubwa amuruhusu asikule vitu hivyo na kujichafua.