Daniel 10:1 — Compare Translations
9 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mnamo mwaka wa tatu wa utawala wa mfalme Koreshi wa Persia, Danieli, aliyeitwa pia Belteshaza, alipewa ufunuo. Ufunuo huo ulikuwa wa kweli, lakini ulikuwa mgumu sana, haukueleweka. Hata hivyo alielewa ufunuo huo maana pia alifahamu maono.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Katika mwaka wa tatu wa utawala wa Koreshi mfalme wa Uajemi, Danieli (ambaye aliitwa Belteshaza) alipewa ufunuo. Ujumbe wake ulikuwa kweli, nao ulihusu vita vikubwa. Ufahamu wa ujumbe ulimjia katika maono.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Katika mwaka wa tatu wa Koreshi, mfalme wa Uajemi, Danieli, ambaye jina lake aliitwa Belteshaza, alifunuliwa neno; na neno lile lilikuwa kweli; maana ni vita vikubwa; naye akalifahamu neno lile, akaelewa na maono hayo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mnamo mwaka wa tatu wa utawala wa mfalme Koreshi wa Persia, Danieli, aliyeitwa pia Belteshaza, alipewa ufunuo. Ufunuo huo ulikuwa wa kweli, lakini ulikuwa mgumu sana, haukueleweka. Hata hivyo alielewa ufunuo huo maana pia alifahamu maono.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Katika mwaka wa tatu wa kutawala kwake Koreshi mfalme wa Uajemi, Danieli (ambaye aliitwa Belteshaza) alipewa ufunuo. Ujumbe wake ulikuwa kweli nao ulihusu vita vikubwa. Ufahamu wa ujumbe ulimjia katika maono.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Katika mwaka wa tatu wa utawala wa Koreshi mfalme wa Uajemi, Danieli (ambaye aliitwa Belteshaza) alipewa ufunuo. Ujumbe wake ulikuwa kweli, nao ulihusu vita vikubwa. Ufahamu wa ujumbe ulimjia katika maono.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Katika mwaka wa tatu wa Kiro, mfalme wa Wapersia, Danieli aliyeitwa jina lake Beltesasari akafunuliwa neno; hilo neno ni la kweli, masumbufu yatakuwa makubwa. Naye akalitambua hilo neno, akayatambua nayo, aliyoyaona.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Katika mwaka wa tatu wa Koreshi, mfalme wa Uajemi, Danieli, ambaye jina lake aliitwa Belteshaza, alifunuliwa neno; na neno lile lilikuwa kweli; maana ni vita vikubwa; naye akalifahamu neno lile, akaelewa na maono hayo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Katika mwaka wa tatu wa utawala wa mufalme Kiro wa Persia, Danieli, aliyeitwa vilevile Beltesaza, alipewa ufunuo. Ufunuo huo ulikuwa wa kweli, lakini ulikuwa mugumu sana. Hata hivyo alielewa ufunuo huo maana alifahamu maono vilevile.