Daniel 10:11 — Compare Translations

9 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Akaniambia, ‘Danieli, wewe unayependwa sana, simama wima usikilize kwa makini maneno nitakayosema, maana nimetumwa kwako.’ Alipokuwa akiniambia maneno haya, mimi nilisimama nikitetemeka.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Akasema, “Danieli, wewe mtu upendwaye sana, fikiri kwa makini maneno ninayoenda kunena nawe; simama wima, kwa maana sasa nimetumwa kwako.” Aliponiambia haya, nikasimama nikitetemeka.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akaniambia, Ee Danieli, mtu upendwaye sana, yafahamu maneno nikuambiayo, ukasimame kiwima-wima; maana kwako nimetumwa sasa. Na aliponiambia neno hili, nalisimama nikitetemeka.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Akaniambia, ‘Danieli, wewe unayependwa sana, simama wima usikilize kwa makini maneno nitakayosema, maana nimetumwa kwako.’ Alipokuwa akiniambia maneno haya, mimi nilisimama nikitetemeka.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Akasema, “Danieli, wewe mtu upendwaye sana, fikiri kwa makini maneno ninayokwenda kunena nawe sasa, simama wima, kwa maana sasa nimetumwa kwako.” Naye aliposema nami haya, nikasimama nikitetemeka.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Akasema, “Danieli, wewe mtu upendwaye sana, fikiri kwa makini maneno ninayokwenda kunena nawe sasa; simama wima, kwa maana sasa nimetumwa kwako.” Naye aliponiambia haya, nikasimama nikitetemeka.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha akaniambia: Danieli, ndiwe mtu wa kupendezwa naye; yatambue hayo maneno, mimi nitakayokuambia, ukisimama hapohapo, unaposimama! kwani nimetumwa kwako. Aliponiambia neno hili, nikainuka na kutetemeka.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akaniambia, Ee Danieli, mtu upendwaye sana, yafahamu maneno nikuambiayo, ukasimame kiwima-wima; maana kwako nimetumwa sasa. Na aliponiambia neno hili, nalisimama nikitetemeka.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Akaniambia: Danieli, wewe unayependwa sana, simama sawa usikilize kwa uangalifu maneno nitakayosema, maana nimetumwa kwako. Alipokuwa akiniambia maneno haya, mimi nilisimama nikitetemeka.