Daniel 10:12 — Compare Translations
9 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ndipo yeye akaniambia, ‘Danieli, usiogope. Mungu alilisikia ombi lako tangu siku ile ya kwanza ulipoamua kujinyenyekesha mbele yake ili upate ufahamu. Mimi nimekuja kwa ajili ya ombi lako hilo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ndipo akaendelea kusema, “Danieli, usiogope. Tangu siku ya kwanza ulipotia moyo wako kupata ufahamu na kujinyenyekeza mbele ya Mungu wako, maneno yako yalisikiwa, nami nimekuja kwa ajili ya maneno yako.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ndipo akaniambia, Usiogope, Danieli; kwa maana tangu siku ile ya kwanza ulipotia moyo wako ufahamu, na kujinyenyekeza mbele za Mungu wako, maneno yako yalisikiwa; nami nimekuja kwa ajili ya maneno yako.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ndipo yeye akaniambia, ‘Danieli, usiogope. Mungu alilisikia ombi lako tangu siku ile ya kwanza ulipoamua kujinyenyekesha mbele yake ili upate ufahamu. Mimi nimekuja kwa ajili ya ombi lako hilo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ndipo akaendelea kusema, “Danieli usiogope. Tangu siku ya kwanza ulipotia moyo wako ili kupata ufahamu na kujinyenyekeza mbele ya Mungu wako, maneno yako yalisikiwa, nami nimekuja kwa ajili ya kuitikia maneno yako.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ndipo akaendelea kusema, “Danieli, usiogope. Tangu siku ya kwanza ulipotia moyo wako ili kupata ufahamu na kujinyenyekeza mbele ya Mungu wako, maneno yako yalisikiwa, nami nimekuja ili kujibu maneno yako.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Akaniambia: Usiogope, Danieli! Kwani tangu siku ya kwanza, ulipojipa moyo wa kutaka utambuzi kwa kujinyenyekeza mbele ya Mungu wako, maneno yako yamesikiwa, nami nimekuja kwa hayo maneno yako.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ndipo akaniambia, Usiogope, Danieli; kwa maana tangu siku ile ya kwanza ulipotia moyo wako ufahamu, na kujinyenyekeza mbele za Mungu wako, maneno yako yalisikiwa; nami nimekuja kwa ajili ya maneno yako.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa hiyo yeye akaniambia: Danieli, usiogope. Mungu alisikia maombi yako tangu siku ile ya kwanza ulipoamua kujinyenyekeza mbele yake kusudi upate ufahamu. Mimi nimekuja kwa ajili ya maombi yako hayo.