Daniel 10:13 — Compare Translations

9 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mkuu wa ufalme wa Persia alinipinga kwa muda wa siku ishirini na moja. Lakini Mikaeli, mmoja wa wakuu, akaja kunisaidia, kwa hiyo nikamwacha huko pamoja na mkuu wa ufalme wa Persia,
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini mkuu wa ufalme wa Uajemi alinipinga kwa siku ishirini na moja. Ndipo Mikaeli, mmoja wa malaika wakuu, alikuja kunisaidia, kwa sababu nilikuwa nimezuiliwa huko na mfalme wa Uajemi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini mkuu wa ufalme wa Uajemi alinipinga siku ishirini na moja; bali, tazama, huyo Mikaeli, mmoja wa hao wakuu wa mbele, akaja kunisaidia; nami nikamwacha huko pamoja na wafalme wa Uajemi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mkuu wa ufalme wa Persia alinipinga kwa muda wa siku ishirini na moja. Lakini Mikaeli, mmoja wa wakuu, akaja kunisaidia, kwa hiyo nikamwacha huko pamoja na mkuu wa ufalme wa Persia,
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini mkuu wa ufalme wa Uajemi alinizuia kwa siku ishirini na moja. Ndipo Mikaeli, mmoja wa hao wakuu, alikuja kunisaidia, kwa sababu nilikuwa nimezuiliwa huko na mfalme wa Uajemi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini mkuu wa ufalme wa Uajemi alinipinga kwa siku ishirini na moja. Ndipo Mikaeli, mmoja wa malaika wakuu, alikuja kunisaidia, kwa sababu nilikuwa nimezuiliwa huko na mfalme wa Uajemi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini mkuu wa ufalme wa Persia akasimama mbele yangu na kunipingia siku ishirini na moja; mara Mikaeli aliye miongoni mwao wakuu wenyewe akaja kunisaidia, nilipokuwa nimeachwa peke yangu kushindana nao wafalme wa Persia.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini mkuu wa ufalme wa Uajemi alinipinga siku ishirini na moja; bali, tazama, huyo Mikaeli, mmoja wa hao wakuu wa mbele, akaja kunisaidia; nami nikamwacha huko pamoja na wafalme wa Uajemi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mukubwa wa ufalme wa Persia alinipinga kwa muda wa siku makumi mbili na moja. Lakini Mikaeli, mumoja kati ya wakubwa, akakuja kunisaidia, kwa hiyo nikamwacha kule pamoja na mukubwa wa ufalme wa Persia,