Daniel 10:19 — Compare Translations

9 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Akaniambia, ‘Usiogope wewe unayependwa sana, uko salama. Uwe imara na hodari.’ Aliposema nami, nilipata nguvu, nikamwambia, ‘Bwana, umekwisha niimarisha; sema kile ulichotaka kusema.’
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Akasema, “Ee mtu upendwaye sana, usiogope. Amani iwe kwako! Uwe na nguvu sasa; jipe nguvu.” Alipozungumza nami, nilipata nguvu, nikasema, “Nena, bwana wangu, kwa kuwa umenipa nguvu.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akasema, Ee mtu upendwaye sana, usiogope; amani na iwe kwako, uwe na nguvu, naam, uwe na nguvu. Aliposema nami nikapata nguvu, nikasema, Ee Bwana wangu, na aseme Bwana wangu; kwa maana umenitia nguvu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Akaniambia, ‘Usiogope wewe unayependwa sana, uko salama. Uwe imara na hodari.’ Aliposema nami, nilipata nguvu, nikamwambia, ‘Bwana, umekwisha niimarisha; sema kile ulichotaka kusema.’
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Akasema, “Ee mtu upendwaye sana, usiogope. Amani iwe kwako! Uwe na nguvu sasa, uwe na nguvu.” Alipozungumza nami, nilipata nguvu nikasema, “Nena, bwana wangu, kwa kuwa umenipa nguvu.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Akasema, “Ee mtu upendwaye sana, usiogope. Amani iwe kwako! Uwe na nguvu sasa; jipe nguvu.” Alipozungumza nami, nilipata nguvu, nikasema, “Nena, bwana wangu, kwa kuwa umenipa nguvu.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
akaniambia: Usiogope! Ndiwe mtu wa kupendezwa naye; tulia tu na kujipa moyo, nguvu zikurudie! Aliponiambia haya, ndipo, nilipopata nguvu, nikamwambia: Bwana wangu na aseme! Kwani umenitia nguvu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akasema, Ee mtu upendwaye sana, usiogope; amani na iwe kwako, uwe na nguvu, naam, uwe na nguvu. Aliposema nami nikapata nguvu, nikasema, Ee Bwana wangu, na aseme Bwana wangu; kwa maana umenitia nguvu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Akaniambia: Usiogope wewe unayependwa sana, uko salama. Ukuwe imara na hodari. Aliposema nami, nilipata nguvu, nikamwambia: Bwana, umekwisha kuniimarisha; sema kile ulichotaka kusema.