Daniel 10:6 — Compare Translations

9 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mwili wake ulingaa kama zabarajadi safi. Uso wake ulifanana na umeme, na macho yake yaliwaka kama miali ya moto. Miguu na mikono yake ilingaa kama shaba iliyosuguliwa sana. Sauti yake ilivuma kama sauti ya umati mkubwa wa watu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mwili wake ulikuwa kama zabarajadi safi, uso wake kama radi, macho yake kama miali wa moto, mikono yake na miguu yake kama mng’ao wa shaba iliyosuguliwa, nayo sauti yake kama ya umati mkubwa wa watu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
mwili wake pia ulikuwa kama zabarajadi safi, na uso wake mfano wa umeme, na macho yake kama taa za moto, na mikono yake na miguu yake rangi yake kama shaba iliyosuguliwa sana, na sauti ya maneno yake kama sauti ya umati wa watu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mwili wake uling'aa kama zabarajadi safi. Uso wake ulifanana na umeme, na macho yake yaliwaka kama miali ya moto. Miguu na mikono yake iling'aa kama shaba iliyosuguliwa sana. Sauti yake ilivuma kama sauti ya umati mkubwa wa watu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mwili wake ulikuwa kama kito cha zabarijadi safi, uso wake kama umeme wa radi, macho yake kama mwali wa moto, mikono yake na miguu yake kama mng'ao wa shaba iliyosuguliwa sana, nayo sauti yake kama ya umati mkubwa wa watu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mwili wake ulikuwa kama kito cha zabarajadi safi, uso wake kama umeme wa radi, macho yake kama mwali wa moto, mikono yake na miguu yake kama mng’ao wa shaba iliyosuguliwa sana, nayo sauti yake kama ya umati mkubwa wa watu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mwili wake ulikuwa kama kito cha Tarsisi, uso wake ulionekana kuwa kama umeme, nayo macho yake yalikuwa kama mienge ya moto, mikono yake na miguu yake ilimerimeta kama shaba iliyokatuliwa, sauti ya kusema kwake ikawa kama uvumi wa watu wengi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
mwili wake pia ulikuwa kama zabarajadi safi, na uso wake mfano wa umeme, na macho yake kama taa za moto, na mikono yake na miguu yake rangi yake kama shaba iliyosuguliwa sana, na sauti ya maneno yake kama sauti ya umati wa watu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mwili wake ulingaa kama zabarajadi safi. Uso wake ulifanana na umeme, na macho yake yaliwaka kama ndimi za moto. Miguu na mikono yake ilingaa kama shaba iliyosafishwa sana. Sauti yake ilivuma kama sauti ya kundi kubwa la watu.