Daniel 10:8 — Compare Translations
9 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hivyo, niliachwa peke yangu nikiangalia hayo maono ya kushangaza. Nguvu zikaniishia, na rangi yangu ikaharibika, nikabaki bila nguvu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa hiyo niliachwa peke yangu, nikitazama maono hayo makubwa; sikubakiwa na nguvu, na rangi ya uso wangu ikabadilika kama aliyekufa, nikakosa nguvu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi nikaachwa peke yangu, nikaona maono haya makubwa, wala hazikubaki nguvu ndani yangu; maana uzuri wangu uligeuzwa ndani yangu kuwa uharibifu, wala sikusaziwa nguvu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hivyo, niliachwa peke yangu nikiangalia hayo maono ya kushangaza. Nguvu zikaniishia, na rangi yangu ikaharibika, nikabaki bila nguvu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa hiyo niliachwa peke yangu, nikikodolea macho maono hayo makubwa, sikubakiwa na nguvu, rangi ya uso wangu ikabadilika kama aliyekufa, nikakosa nguvu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa hiyo niliachwa peke yangu, nikikodolea macho maono hayo makubwa; sikubakiwa na nguvu, na rangi ya uso wangu ikabadilika kama aliyekufa, nikakosa nguvu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mimi nikasalia peke yangu, nami nilipoyaona hayo makuu, yalivyooneka, haikusalia nguvu mwangu, nayo yaliyokuwa mazuri kwangu yakageuka kuwa mabaya, nguvu zangu zikanipotea kabisa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi nikaachwa peke yangu, nikaona maono haya makubwa, wala hazikubaki nguvu ndani yangu; maana uzuri wangu uligeuzwa ndani yangu kuwa uharibifu, wala sikusaziwa nguvu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Hivyo, niliachwa peke yangu nikiangalia hayo maono ya kushangaza. Nguvu zikaniishia, na uso wangu ukabadilika rangi, nikabaki bila nguvu.