Daniel 11:10 — Compare Translations
9 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“ ‘Wana wa mfalme wa kaskazini watakusanya jeshi kubwa na kujiandaa kwa vita. Jeshi hilo litasonga mbele kama mafuriko litapita na kupigana vita mpaka ngome ya adui.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wana wa mfalme wa Kaskazini watajiandaa kwa vita na kukusanya jeshi kubwa, ambalo litafagia nchi kama mafuriko yasiyozuilika, na kuendelea na vita hadi kwenye ngome ya mfalme wa Kusini.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na wanawe watafanya vita, na kukusanya mkutano wa majeshi makuu; watakaokuja na kufurika na kupita katikati; nao watarudi na kufanya vita mpaka penye ngome yake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“‘Wana wa mfalme wa kaskazini watakusanya jeshi kubwa na kujiandaa kwa vita. Jeshi hilo litasonga mbele kama mafuriko litapita na kupigana vita mpaka ngome ya adui.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hata hivyo, wana wa mfalme wa Kaskazini watajiandaa kwa vita na kukusanya jeshi kubwa, ambalo litafagia nchi kama mafuriko yasiyozuilika na kuendelea na vita hadi kwenye ngome ya mfalme wa Kusini.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wana wa mfalme wa Kaskazini watajiandaa kwa vita na kukusanya jeshi kubwa, ambalo litafagia nchi kama mafuriko yasiyozuilika na kuendelea na vita hadi kwenye ngome ya mfalme wa Kusini.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini wanawe watatengeneza vita wakikusanya vikosi vingi mno vivumavyo; kisha mmoja atakwenda kuifurikia na kuieneza hiyo nchi, katika safari ya pili atapeleka vita mpaka bomani kwake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na wanawe watafanya vita, na kukusanya mkutano wa majeshi makuu; watakaokuja na kufurika na kupita katikati; nao watarudi na kufanya vita mpaka penye ngome yake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wana wa mufalme wa kaskazini watakusanya kundi kubwa la waaskari na kujitayarisha kwa vita. Kundi hilo litasonga mbele kama mafuriko ya maji litapita na kupigana vita mpaka ndani ya muji wenye kuta wa waadui.