Daniel 11:12 — Compare Translations

9 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Baada ya kulishinda vibaya jeshi la kaskazini na kuua maelfu, ataanza kujisifu, ila hataendelea kuwa mshindi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Jeshi litakapotekwa, mfalme wa Kusini atajawa na kiburi, na atachinja maelfu mengi; hata hivyo hatabaki na ushindi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Atakapokwisha kuchukua lile jeshi, moyo wake utatukuzwa; naye atawaangusha makumi elfu; lakini hataongezewa nguvu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Baada ya kulishinda vibaya jeshi la kaskazini na kuua maelfu, ataanza kujisifu, ila hataendelea kuwa mshindi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakati jeshi litakapokuwa limechukuliwa, mfalme wa Kusini atajawa na majivuno na atachinja maelfu mengi, hata hivyo hatabaki na ushindi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wakati jeshi litakapokuwa limechukuliwa, mfalme wa Kusini atajawa na kiburi na atachinja maelfu mengi, hata hivyo hatabaki na ushindi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
ndipo, vitakapochukuliwa, ingawa viwe vingi. Naye moyo wake utajikuza, lakini hatashinda kabisa, ijapo aangushe maelfu na maelfu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Atakapokwisha kuchukua lile jeshi, moyo wake utatukuzwa; naye atawaangusha makumi elfu; lakini hataongezewa nguvu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha kulishinda vibaya kundi la waasakri wa kaskazini na kuua maelfu, ataanza kujisifu, lakini hataendelea kuwa mushindi.