Daniel 11:13 — Compare Translations
9 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“ ‘Maana mfalme wa kaskazini baadaye ataandaa jeshi kubwa kuliko lile la awali. Kisha baada ya miaka kadhaa atarudi na jeshi kubwa lenye vifaa vingi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa maana mfalme wa Kaskazini atakusanya jeshi kubwa kuliko lile la kwanza; baada ya miaka kadhaa, atasonga mbele na jeshi kubwa mno lililoandaliwa vizuri.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa maana mfalme wa kaskazini atarudi, naye atapanga jeshi kubwa kuliko lile la kwanza; naye hakika atakuja mwisho wa zamani zile, yaani, baada ya miaka kadha wa kadha, pamoja na jeshi kubwa na mali nyingi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“‘Maana mfalme wa kaskazini baadaye ataandaa jeshi kubwa kuliko lile la awali. Kisha baada ya miaka kadhaa atarudi na jeshi kubwa lenye vifaa vingi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa maana mfalme wa Kaskazini atakusanya jeshi jingine, kubwa kuliko lile la kwanza, na baada ya miaka kadha wa kadha, atasonga mbele na jeshi kubwa mno lililoandaliwa vizuri.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa maana mfalme wa Kaskazini atakusanya jeshi jingine kubwa kuliko lile la kwanza; na baada ya miaka kadha, atasonga mbele na jeshi kubwa mno lililoandaliwa vizuri.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mfalme wa kaskazini atarudi na kuleta vikosi vilivyo vingi kuliko vile vya kwanza. Siku nyingi na miaka itakapopita, atakuja navyo hivyo vikosi vikubwa vyenye mata mengi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa maana mfalme wa kaskazini atarudi, naye atapanga jeshi kubwa kuliko lile la kwanza; naye hakika atakuja mwisho wa zamani zile, yaani, baada ya miaka kadha wa kadha, pamoja na jeshi kubwa na mali nyingi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Maana kwa mwisho mufalme wa kaskazini atatayarisha kundi kubwa la waaskari kuliko lile la mbele. Kisha miaka michache atarudi na kundi kubwa la waaskari lenye vifaa vingi vya vita.