Daniel 11:14 — Compare Translations
9 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wakati huo watu wengi watamwasi mfalme wa kusini. Baadhi ya watu wakatili wa taifa lako Danieli, wataasi ili kutekeleza maono haya, lakini hawatafaulu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Katika nyakati hizo, wengi watainuka dhidi ya mfalme wa Kusini. Watu wenye ghasia miongoni mwa watu wako mwenyewe wataasi ili kutimiza maono, lakini bila mafanikio.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na zamani zile watu wengi watasimama ili kumpinga mfalme wa kusini; pia, wenye jeuri miongoni mwa watu wako watajiinua ili kuyathibitisha maono; lakini wataanguka.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wakati huo watu wengi watamwasi mfalme wa kusini. Baadhi ya watu wakatili wa taifa lako Danieli, wataasi ili kutekeleza maono haya, lakini hawatafaulu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Katika nyakati hizo wengi watainuka dhidi ya mfalme wa Kusini. Watu wenye ghasia miongoni mwa watu wako mwenyewe wataasi ili kutimiza maono, lakini bila mafanikio.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Katika nyakati hizo wengi watainuka dhidi ya mfalme wa Kusini. Watu wenye ghasia miongoni mwa watu wako mwenyewe wataasi ili kutimiza maono, lakini bila mafanikio.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Siku hizo wengi watamwinukia mfalme wa kusini, hata wana wao walio ukoo wako wenye ukorofi watainuka, wayatimize mambo uliyoyaona, lakini watajikwaa, waanguke.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na zamani zile watu wengi watasimama ili kumpinga mfalme wa kusini; pia, wenye jeuri miongoni mwa watu wako watajiinua ili kuyathibitisha maono; lakini wataanguka.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wakati huo watu wengi watamwasi mufalme wa kusini. Watu wamoja waovu wa taifa lako wewe Danieli, wataasi kwa kutimiza maono haya, lakini watashindwa.