Daniel 11:15 — Compare Translations
9 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ndipo mfalme wa kaskazini atauzingira mji wenye ngome imara na kuuteka. Wanajeshi wa kusini hawatastahimili, hata wale wateule, maana hawatakuwa na nguvu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ndipo mfalme wa Kaskazini atakuja na kuuzingira mji kwa majeshi, na kuuteka mji wa ngome. Majeshi ya Kusini yatakosa nguvu za kumzuia; naam, hata vikosi vyao vya askari vilivyo bora zaidi, havitakuwa na nguvu za kuwakabili.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi mfalme wa kaskazini atakuja, na kufanya kilima, na kuupiga mji wenye maboma; na silaha za kusini hazitaweza kumpinga, wala watu wake wateule, wala hapatakuwa na nguvu za kumpinga.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ndipo mfalme wa kaskazini atauzingira mji wenye ngome imara na kuuteka. Wanajeshi wa kusini hawatastahimili, hata wale wateule, maana hawatakuwa na nguvu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ndipo mfalme wa Kaskazini atakuja na kuuzunguka mji kwa majeshi na kuuteka mji uliozungushiwa boma. Majeshi ya Kusini yatakosa nguvu ya kuyazuia, naam, hata vikosi vyao vya askari vilivyo bora kuliko vingine, havitakuwa na nguvu ya kuwakabili.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ndipo mfalme wa Kaskazini atakuja na kuuzunguka mji kwa majeshi, na kuuteka mji wa ngome. Majeshi ya Kusini yatakosa nguvu za kuyazuia; naam, hata vikosi vyao vya askari vilivyo bora zaidi, havitakuwa na nguvu ya kuwakabili.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, mfalme wa kaskazini atakapokuja, atamzungushia ukingo wa mchanga, auteke mji wake ulio na boma. Ndipo, itakapokuwa, mikono yao wakusini isishupae, hata mafundi wake wa vita wasiwe na nguvu za kusimama.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi mfalme wa kaskazini atakuja, na kufanya kilima, na kuupiga mji wenye maboma; na silaha za kusini hazitaweza kumpinga, wala watu wake wateule, wala hapatakuwa na nguvu za kumpinga.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Halafu mufalme wa kaskazini atalundika udongo kando ya muji wenye kuta imara na kuuteka. Waaskari wa kusini hawataweza kuupiganisha, hata wale wafundi wa vita, maana hawatakuwa na nguvu.