Daniel 11:16 — Compare Translations

9 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mvamizi atawatenda kama apendavyo, hakuna atakeyethubutu kupingana naye. Atasimama katika nchi tukufu, na nchi hiyo yote itakuwa chini ya mamlaka yake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Huyo mvamia nchi atafanya apendavyo; hakuna yeyote atakayeweza kumpinga. Atajiimarisha katika Nchi ya Kupendeza, na atakuwa na uwezo wa kuiangamiza.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Maana ajaye kupigana naye atatenda kadiri apendavyo, wala hapana mtu atakayesimama mbele yake; naye atasimama katika nchi ya uzuri, na uharibifu utakuwa mkononi mwake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mvamizi atawatenda kama apendavyo, hakuna atakeyethubutu kupingana naye. Atasimama katika nchi tukufu, na nchi hiyo yote itakuwa chini ya mamlaka yake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Huyo avamiaye nchi kwa vita atafanya apendavyo, hakuna ye yote atakayeweza kusimama mbele yake. Atajiimarisha mwenyewe katika Nchi ya Kupendeza na atakuwa na uwezo wa kuiangamiza.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Huyo mvamia nchi atafanya apendavyo; hakuna yeyote atakayeweza kumpinga. Atajiimarisha katika Nchi ya Kupendeza, na atakuwa na uwezo wa kuiangamiza.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Naye yeye amjiaye atafanya, kama anavyopendezwa, kwani hatakuwako atakayesimama mbele yake. Hata katika nchi hiyo yenye utukufu atakaa, mikono yake ikiiangamiza.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Maana ajaye kupigana naye atatenda kadiri apendavyo, wala hapana mtu atakayesimama mbele yake; naye atasimama katika nchi ya uzuri, na uharibifu utakuwa mkononi mwake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mushambulizi atawatendea sawa anavyopenda; hakuna atakeyesubutu kupingana naye. Atasimama katika inchi tukufu, na inchi hiyo yote itakuwa chini ya mamlaka yake.

Recommended Reading