Daniel 11:17 — Compare Translations
9 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“ ‘Huyo mvamizi atakusudia kuja na jeshi lake lote, naye atafanya mapatano na kuyatekeleza. Atamwoza binti mmoja ili kuuangamiza ufalme wa adui yake; lakini mpango wake hautafaulu, wala kumfaidia lolote.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ataamua kuja na nguvu za ufalme wake wote, na kufanya mapatano ya amani na mfalme wa Kusini. Naye atamtoa binti yake aolewe naye ili kuuangusha ufalme, lakini mipango yake haitafanikiwa wala kumsaidia.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naye atakaza uso wake ili aje pamoja na nguvu zote za ufalme wake, naye atafanya mapatano naye; naye atatenda kadiri apendavyo; naye atampa binti wa watu ili amharibu; lakini hilo halitasimama wala kumfaa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“‘Huyo mvamizi atakusudia kuja na jeshi lake lote, naye atafanya mapatano na kuyatekeleza. Atamwoza binti mmoja ili kuuangamiza ufalme wa adui yake; lakini mpango wake hautafaulu, wala kumfaidia lolote.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Naye atafanya mipango kuja na nguvu za ufalme wake wote na kufanya mapatano ya amani na mfalme wa Kusini. Naye atamtoa binti yake aolewe naye ili kufanya mipango ya kuuangusha ufalme ndani kwa ndani, lakini mipango haitafanikiwa wala kumsaidia.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ataamua kuja na nguvu za ufalme wake wote na kufanya mapatano ya amani na mfalme wa Kusini. Naye atamtoa binti yake aolewe naye ili kuuangusha ufalme, lakini mipango yake haitafanikiwa wala kumsaidia.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha atauelekeza uso wake kuja huko na enzi yote ya ufalme wake, afanye mapatano naye akimpa mwanawe, awe mkewe, aiangamize nchi hiyo, lakini jambo hili halitakuwa, hatafanikiwa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naye atakaza uso wake ili aje pamoja na nguvu zote za ufalme wake, naye atafanya mapatano naye; naye atatenda kadiri apendavyo; naye atampa binti wa watu ili amharibu; lakini hilo halitasimama wala kumfaa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Huyo mushambulizi atakusudia kuja na kundi lake lote la waaskari, naye atafanya mapatano na kuyatimiza. Atamuoesha binti yake mumoja kusudi apate kuuangamiza ufalme wa adui yake; lakini mupango wake hautawezekana, wala kumufaidia kwa jambo lolote.