Daniel 11:18 — Compare Translations

9 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Baadaye, atazigeukia na kuzishambulia nchi nyingi za pwani na kuzishinda. Lakini jemadari mgeni atamshinda na kuyakomesha majivuno yake mwenyewe; naam, atamrudishia mfalme wa kaskazini majivuno yake mwenyewe.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ndipo atabadili nia yake na kupigana na nchi za pwani na aziteke nyingi, lakini jemadari mmoja atakomesha ufidhuli wake, na kurudisha ufidhuli wake juu yake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Baada ya hayo atauelekeza uso wake kwenye visiwa, naye atavipiga visiwa vingi; lakini mkuu mmoja ataikomesha aibu iliyoletwa na yeye; naam, aibu yake hiyo atamrudishia mwenyewe.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Baadaye, atazigeukia na kuzishambulia nchi nyingi za pwani na kuzishinda. Lakini jemadari mgeni atamshinda na kuyakomesha majivuno yake mwenyewe; naam, atamrudishia mfalme wa kaskazini majivuno yake mwenyewe.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ndipo atabadili mwelekeo wake kuelekea nchi za pwani na ataziteka nyingi, lakini jemadari kutoka mahali pengine atakomesha ufidhuli wake na kurudisha ufidhuli wake juu yake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ndipo atabadili nia yake kupigana na nchi za pwani na ataziteka nyingi, lakini jemadari mmoja atakomesha ufidhuli wake na kurudisha ufidhuli wake juu yake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha atauelekeza uso wake kwenda kupiga vita katika nchi za baharini, nazo nyingi ataziteka. Lakini huko kutakuwa na mpiga vita atakayeyakomesha matusi yake, asitukane tena, akimlipisha hayo matusi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Baada ya hayo atauelekeza uso wake kwenye visiwa, naye atavipiga visiwa vingi; lakini mkuu mmoja ataikomesha aibu iliyoletwa na yeye; naam, aibu yake hiyo atamrudishia mwenyewe.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nyuma ya hayo, atageukia na kushambulia inchi nyingi za kandokando ya bahari na kuzishinda. Lakini jemadari mugeni atamushinda na kuyakomesha majivuno yake mwenyewe; kweli atamurudishia mufalme wa kaskazini majivuno yake mwenyewe.