Daniel 11:2 — Compare Translations
9 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Sasa nitakueleza ule ukweli wa mambo haya. “ ‘Tazama, wafalme wengine watatu wataitawala nchi ya Persia. Hao watafuatwa na mfalme wa nne ambaye atakuwa tajiri kuliko wale waliomtangulia. Wakati wa kilele cha nguvu na utajiri wake, ataanza kuushambulia ufalme wa Ugiriki.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Sasa basi, ninakuambia kweli: Wafalme wengine watatu watatokea Uajemi. Kisha atatokea mfalme wa nne, ambaye atakuwa tajiri sana kuliko wengine wote. Atakapokuwa amekwisha kujipatia nguvu kwa utajiri wake, atamchochea kila mmoja dhidi ya ufalme wa Uyunani.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nami sasa nitakuonyesha yaliyo kweli. Tazama, watasimama wafalme watatu katika Uajemi; naye mfalme wa nne atakuwa tajiri kuliko hao wote; naye atakapopata nguvu kwa utajiri wake, atawachochea wote juu ya ufalme wa Uyunani.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Sasa nitakueleza ule ukweli wa mambo haya. “‘Tazama, wafalme wengine watatu wataitawala nchi ya Persia. Hao watafuatwa na mfalme wa nne ambaye atakuwa tajiri kuliko wale waliomtangulia. Wakati wa kilele cha nguvu na utajiri wake, ataanza kuushambulia ufalme wa Ugiriki.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Sasa basi, ninakuambia kweli: Wafalme watatu zaidi watatokea Uajemi, kisha atatokea mfalme wa nne, ambaye atakuwa tajiri sana kuliko wengine wote. Wakati atakapokuwa amekwisha kujipatia nguvu kwa utajiri wake, atamchochea kila mmoja dhidi ya ufalme wa Uyunani.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Sasa basi, ninakuambia kweli: Wafalme watatu zaidi watatokea Uajemi, kisha atatokea mfalme wa nne, ambaye atakuwa tajiri sana kuliko wengine wote. Wakati atakapokuwa amekwisha kujipatia nguvu kwa utajiri wake, atamchochea kila mmoja dhidi ya ufalme wa Uyunani.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Sasa nitakuonyesha yatakayokuwa kweli: Tazama, watandokea bado wafalme watatu wa Persia, wa nne atakuwa mwenye mali nyingi sana kuliko wote; kwa hizo nguvu zake, atakazozipata kwa mali zake nyingi, atawainua wote kuuendea ufalme wa Ugriki.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nami sasa nitakuonyesha yaliyo kweli. Tazama, watasimama wafalme watatu katika Uajemi; naye mfalme wa nne atakuwa tajiri kuliko hao wote; naye atakapopata nguvu kwa utajiri wake, atawachochea wote juu ya ufalme wa Uyunani.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Sasa nitakuelezea ule ukweli wa mambo haya. Wafalme wengine watatu wataitawala inchi ya Persia. Hao watafuatwa na mufalme wa ine ambaye atakuwa tajiri kuliko wale waliomutangulia. Wakati atakapopata nguvu kwa ajili ya utajiri wake, ataanza kuushambulia ufalme wa Ugriki.