Daniel 11:20 — Compare Translations

9 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“ ‘Huyu atafuatwa na mfalme mwingine ambaye atatuma mtozaushuru kupitia katika fahari ya ufalme wake. Mfalme huyo atauawa baada ya siku chache, lakini si kwa hasira wala vitani.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Atakayetawala baada yake atamtuma mtoza ushuru ili kudumisha fahari ya kifalme. Hata hivyo, baada ya miaka michache ataangamizwa, lakini si katika hasira wala katika vita.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ndipo badala yake atasimama mmoja, atakayepitisha mwenye kutoza ushuru kati ya utukufu wa ufalme wake; lakini katika muda wa siku chache ataangamizwa, si kwa hasira, wala si katika vita.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“‘Huyu atafuatwa na mfalme mwingine ambaye atatuma mtozaushuru kupitia katika fahari ya ufalme wake. Mfalme huyo atauawa baada ya siku chache, lakini si kwa hasira wala vitani.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Atakayetawala baada yake atamtuma mtoza ushuru ili kudumisha fahari ya kifalme. Hata hivyo, kwa miaka michache ataangamizwa, lakini si katika hasira wala katika vita.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Atakayetawala baada yake atamtuma mtoza ushuru ili kudumisha fahari ya kifalme. Hata hivyo, baada ya miaka michache ataangamizwa, lakini si katika hasira wala katika vita.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mahali pake ataondokea mwingine atakayetuma mtoza kodi penye utukufu wa ufalme wake; lakini kwa muda wa siku chache atavunjwa, lakini haitakuwa kwa ukali wa mtu wala kwa mapigano.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ndipo badala yake atasimama mmoja, atakayepitisha mwenye kutoza ushuru kati ya utukufu wa ufalme wake; lakini katika muda wa siku chache ataangamizwa, si kwa hasira, wala si katika vita.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Huyu atafuatwa na mufalme mwingine ambaye atatuma mulipishaji wa kodi kupita katika nafasi ya utukufu ya ufalme wake. Mufalme huyo atauawa kisha siku chache, lakini si kwa hasira wala katika vita.