Daniel 11:21 — Compare Translations

9 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“ ‘Mfalme atakayefuata atakuwa baradhuli ambaye hana idhini ya kushika ufalme, naye atakuja bila taarifa na kunyakua ufalme kwa hila.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Atakayetawala baada yake atakuwa mtu wa kudharauliwa ambaye hajapewa heshima ya kifalme. Atauvamia ufalme wakati watu wake wanapojiona kuwa salama, naye atautwaa kwa hila.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kisha badala yake atasimama mmoja, mtu astahiliye kudharauliwa, ambaye hawakumpa heshima ya ufalme; naye atakuja wakati wa amani, naye ataupata ufalme kwa kujipendekeza.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“‘Mfalme atakayefuata atakuwa baradhuli ambaye hana idhini ya kushika ufalme, naye atakuja bila taarifa na kunyakua ufalme kwa hila.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Atakayetawala baada yake atakuwa mtu wa kudharauliwa ambaye hajapewa heshima ya kifalme. Atauvamia ufalme wakati watu wake wanapojiona wako salama, naye atautwaa kwa hila.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Atakayetawala baada yake atakuwa mtu wa kudharauliwa ambaye hajapewa heshima ya kifalme. Atauvamia ufalme wakati watu wake wanapojiona wako salama, naye atautwaa kwa hila.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mahali pake ataondokea mtu abezwaye, wasiyempa macheo ya ufalme; naye atauingia kwa kuja kwa upole, aushike ufalme kwa kujitendekeza na kusema maneno matamu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kisha badala yake atasimama mmoja, mtu astahiliye kudharauliwa, ambaye hawakumpa heshima ya ufalme; naye atakuja wakati wa amani, naye ataupata ufalme kwa kujipendekeza.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mufalme atakayefuata atakuwa wa kuzarauliwa ambaye asiyeweza kupewa heshima ya kifalme, naye atakuja wakati watu wasiouzania na kunyanganya ufalme kwa werevu.