Daniel 11:24 — Compare Translations
9 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Bila taarifa atazivamia sehemu za mkoa zenye utajiri mwingi na kufanya mambo ambayo hayakufanywa hata na mmoja wa wazee wake waliomtangulia. Kisha, atawagawia wafuasi wake mateka, mali na vitu alivyoteka nyara vitani. Atafanya mipango ya kuzishambulia ngome, lakini kwa muda tu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wakati majimbo yaliyo tajiri sana yanajiona salama, atayavamia, naye atatimiza kile baba zake na babu zake hawakuweza. Atagawa nyara, mateka na utajiri miongoni mwa wafuasi wake. Atapanga njama ya kupindua miji yenye ngome, lakini kwa muda mfupi tu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wakati wa amani atapaingia mahali palipofanikiwa sana pa wilaya hiyo; naye atatenda mambo ambayo baba zake hawakuyatenda, wala babu zake; atatawanya kati yao mawindo, na mateka, na mali; naam, atatunga hila zake juu ya ngome, hata wakati ulioamriwa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Bila taarifa atazivamia sehemu za mkoa zenye utajiri mwingi na kufanya mambo ambayo hayakufanywa hata na mmoja wa wazee wake waliomtangulia. Kisha, atawagawia wafuasi wake mateka, mali na vitu alivyoteka nyara vitani. Atafanya mipango ya kuzishambulia ngome, lakini kwa muda tu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakati majimbo yaliyo tajiri sana yanapojiona salama, atayavamia naye atafanikisha kile ambacho baba zake wala babu zake hawakufanya. Atagawa nyara, mateka na utajiri miongoni mwa wafuasi wake. Atafanya hila ya kupindua miji yenye maboma, lakini kwa muda mfupi tu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wakati majimbo yaliyo tajiri sana yanajiona salama, atayavamia, naye atafanikisha kile ambacho baba zake wala babu zake hawakuweza. Atagawa nyara, mateka na utajiri miongoni mwa wafuasi wake. Atafanya hila ya kupindua miji yenye maboma, lakini kwa muda mfupi tu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwa upole ataziingia nchi zenye manono, afanye mambo, wasiyoyafanya baba zake wala baba za baba zake, akitapanya kwao mapokonyo na mateka na mali zo zote, miji yenye maboma akiiwazia mizungu ya kuipata, lakini vitakuwa siku hizo tu zilizokatwa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wakati wa amani atapaingia mahali palipofanikiwa sana pa wilaya hiyo; naye atatenda mambo ambayo baba zake hawakuyatenda, wala babu zake; atatawanya kati yao mawindo, na mateka, na mali; naam, atatunga hila zake juu ya ngome, hata wakati ulioamriwa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Na kwa wakati wasiouwazia ataingia katika sehemu za jimbo zenye utajiri mwingi na kufanya mambo ambayo hayakufanyika hata na mumoja wa babu zake waliomutangulia. Kisha, atawagawanyia wafuasi wake mali na vitu alivyonyanganya katika vita. Atafanya mipango ya kuishambulia miji yenye kuta, lakini kwa muda tu.