Daniel 11:25 — Compare Translations
9 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“ ‘Kwa ujasiri mwingi, ataunda jeshi kubwa ili kuushambulia ufalme wa kusini, naye mfalme wa kusini atajibu mashambulizi hayo kwa jeshi kubwa zaidi na lenye nguvu sana. Lakini, mfalme wa kusini hatafaulu kwani mipango ya hila itafanywa dhidi yake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Atachochea nguvu zake na ushujaa wake kwa jeshi kubwa dhidi ya mfalme wa Kusini. Mfalme wa Kusini atafanya vita na jeshi kubwa lenye nguvu sana, lakini hataweza kusimama kwa sababu ya hila zilizopangwa dhidi yake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naye atachochea nguvu zake na ushujaa wake juu ya huyo mfalme wa kusini kwa jeshi kubwa; na mfalme wa kusini atafanya vita kwa jeshi kubwa mno lenye nguvu nyingi; lakini hatasimama; maana watatunga hila juu yake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“‘Kwa ujasiri mwingi, ataunda jeshi kubwa ili kuushambulia ufalme wa kusini, naye mfalme wa kusini atajibu mashambulizi hayo kwa jeshi kubwa zaidi na lenye nguvu sana. Lakini, mfalme wa kusini hatafaulu kwani mipango ya hila itafanywa dhidi yake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Pamoja na jeshi kubwa atachochea nguvu zake na ushujaa wake dhidi ya mfalme wa Kusini. Mfalme wa Kusini atafanya vita na jeshi lenye nguvu sana, lakini hataweza kusimama kwa sababu ya mashauri yaliyofanywa kwa hila dhidi yake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Pamoja na jeshi kubwa atachochea nguvu zake na ushujaa wake dhidi ya mfalme wa Kusini. Mfalme wa Kusini atafanya vita na jeshi lenye nguvu sana, lakini hataweza kusimama kwa sababu ya kwa hila zilizofanywa dhidi yake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha ataviinua vikosi vyake kwa kujipa moyo wa kumwendea mfalme wa kusini kwa hizo nguvu kuu za vikosi vyake. Naye mfalme wa kusini atatengeneza vita na kuvipanga vikosi vyake vikubwa vilivyo vyenye nguvu kabisa, lakini hatashinda; kwani watakaomwazia mawazo ya njama
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naye atachochea nguvu zake na ushujaa wake juu ya huyo mfalme wa kusini kwa jeshi kubwa; na mfalme wa kusini atafanya vita kwa jeshi kubwa mno lenye nguvu nyingi; lakini hatasimama; maana watatunga hila juu yake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa uhodari mwingi, ataunda kundi kubwa la waaskari kusudi apate kuushambulia ufalme wa kusini, naye mufalme wa kusini atajibu mashambulizi hayo kwa kundi kubwa zaidi la waaskari na lenye nguvu sana. Lakini, mufalme wa kusini hatashinda kwa maana watafanya shauri baya juu yake.