Daniel 11:26 — Compare Translations

9 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wale wanaokula pamoja naye, ndio watakaomwangamiza. Watamwangamiza na jeshi lake litafagiliwa mbali na wengi watauawa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wale wanaokula kutoka meza ya mfalme watajaribu kumwangamiza; jeshi lake litafagiliwa mbali, nao wengi watakufa vitani.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naam, walao sehemu ya chakula chake watamwangamiza, na jeshi lake litagharikishwa; na wengi wataanguka wameuawa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wale wanaokula pamoja naye, ndio watakaomwangamiza. Watamwangamiza na jeshi lake litafagiliwa mbali na wengi watauawa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wale wanaokula kutoka kwenye ruzuku za mfalme watajaribu kumwangamiza, jeshi lake litafagiliwa mbali, nao wengi watakufa vitani.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wale wanaokula kutoka kwenye ruzuku za mfalme watajaribu kumwangamiza; jeshi lake litafagiliwa mbali, nao wengi watakufa vitani.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
ndio wanaokula naye vilaji vyake vya urembo; wao ndio watakaomvunja, vikosi vyake navyo vitatawanyika po pote, wengi wao watakufa kwa kuumizwa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naam, walao sehemu ya chakula chake watamwangamiza, na jeshi lake litagharikishwa; na wengi wataanguka wameuawa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wale wanaokula pamoja naye, ndio watakaomwangamiza. Watamwangamiza na waaskari wake watasambazwa na wengi watauawa.