Daniel 11:31 — Compare Translations

9 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wanajeshi wake watalitia najisi hekalu na ngome zake, watakomesha tambiko za kuteketezwa kila siku na kusimamisha huko hekaluni chukizo haribifu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Majeshi yake yenye silaha yatainuka ili kunajisi ngome ya Hekalu, na kuondolea mbali sadaka ya kuteketezwa ya kila siku. Ndipo watalisimamisha chukizo la uharibifu linalosababisha ukiwa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na wenye silaha watasimama upande wake, nao watapatia unajisi mahali patakatifu, ndiyo ngome, nao wataondoa sadaka ya kuteketezwa ya kila siku, nao watalisimamisha chukizo la uharibifu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wanajeshi wake watalitia najisi hekalu na ngome zake, watakomesha tambiko za kuteketezwa kila siku na kusimamisha huko hekaluni chukizo haribifu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Majeshi yake yenye silaha yatainuka ili kunajisi ngome ya Hekalu na kuondolea mbali sadaka ya kuteketezwa ya kila siku. Ndipo watalisimamisha chukizo la uharibifu lisababishalo ukiwa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Majeshi yake yenye silaha yatainuka ili kunajisi ngome ya Hekalu, na kuondolea mbali sadaka ya kuteketezwa ya kila siku. Ndipo watalisimamisha chukizo la uharibifu lisababishalo ukiwa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha mikono yao, aliowaweka huko, itapachafua Patakatifu palipokuwa boma la nguvu, watayakomesha matambiko ya kila siku, kisha wataweka hapo mwangamizaji atapishaye.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na wenye silaha watasimama upande wake, nao watapatia unajisi mahali patakatifu, ndiyo ngome, nao wataondoa sadaka ya kuteketezwa ya kila siku, nao watalisimamisha chukizo la uharibifu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Waaskari wake watalichafua hekalu na kuta zake, watakomesha sadaka za kuteketezwa kwa moto za kila siku na kusimamisha kule katika hekalu chukizo linaloleta uharibifu.