Daniel 11:32 — Compare Translations

9 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Atawashawishi kwa hila wale walioasi agano, lakini watu walio waaminifu kwa Mungu wao watasimama imara na kuchukua hatua.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa udanganyifu, atapotosha wale walionajisi agano, lakini watu wanaomjua Mungu wao watampinga kwa uthabiti.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na wao wafanyao maovu juu ya hilo agano atawapotosha kwa maneno ya kujipendekeza; lakini watu wamjuao Mungu wao watakuwa hodari, na kutenda mambo makuu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Atawashawishi kwa hila wale walioasi agano, lakini watu walio waaminifu kwa Mungu wao watasimama imara na kuchukua hatua.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa udanganyifu atapotosha wale walionajisi Agano, lakini watu wanaomjua Mungu wao watampinga kwa uthabiti.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa udanganyifu atapotosha wale walionajisi agano, lakini watu wanaomjua Mungu wao watampinga kwa uthabiti.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nao walioacha kulicha lile Agano atawashurutisha kwa maneno madanganyifu, wamwache naye Mungu, lakini hao wamjuao Mungu wao watajipatia nguvu za kufanya yawapasayo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na wao wafanyao maovu juu ya hilo agano atawapotosha kwa maneno ya kujipendekeza; lakini watu wamjuao Mungu wao watakuwa hodari, na kutenda mambo makuu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Atawashawishi kwa werevu wale walioasi agano, lakini watu wanaokuwa waaminifu kwa Mungu wao watasimama imara na kutenda.