Daniel 11:36 — Compare Translations

9 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“ ‘Mfalme atafanya kama apendavyo. Atajitukuza na kujikweza kwamba yeye ni mkuu kuliko miungu yote, na kumkufuru Mungu wa miungu. Ataendelea kufanikiwa mpaka ghadhabu ifikie kikomo chake, kwani yaliyopangwa lazima yatimie.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Mfalme atafanya apendavyo. Atajikweza na kujitukuza juu ya kila mungu, naye atasema mambo ambayo hayajawahi kusikiwa dhidi ya Mungu wa miungu. Atafanikiwa hadi wakati wa ghadhabu utimie, kwa maana kile kilichokusudiwa lazima kitatukia.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naye mfalme atafanya kama apendavyo; naye atajitukuza na kujiadhimisha juu ya kila mungu, naye atanena maneno ya ajabu juu ya Mungu wa miungu, naye atafanikiwa mpaka ghadhabu itakapotimia; maana yaliyokusudiwa yatafanyika.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“‘Mfalme atafanya kama apendavyo. Atajitukuza na kujikweza kwamba yeye ni mkuu kuliko miungu yote, na kumkufuru Mungu wa miungu. Ataendelea kufanikiwa mpaka ghadhabu ifikie kikomo chake, kwani yaliyopangwa lazima yatimie.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Mfalme atafanya apendavyo. Atajikweza na kujitukuza mwenyewe kujihesabu mwenye nguvu zaidi juu ya kila mungu naye atasema vitu ambavyo havijasikiwa dhidi ya Mungu wa miungu. Atafanikiwa hadi wakati wa ghadhabu utimie, kwa maana kile kilichokusudiwa lazima kitokee.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Mfalme atafanya apendavyo. Atajikweza na kujitukuza juu ya kila mungu, naye atasema mambo ambayo hayajasikiwa dhidi ya Mungu wa miungu. Atafanikiwa hadi wakati wa ghadhabu utimie, kwa maana kile kilichokusudiwa lazima kitokee.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mfalme yule atafanya, kama anavyopendezwa, atajivuna na kujiwazia kuwa mkuu kuliko mungu wo wote, aseme maneno ya kustaajabisha kwa kumbeza naye Mungu aishindaye miungu; naye atayaendesha mambo hayo, mpaka siku za makali zitakapotimia, k kwani aliyotakiwa hayana budi kufanyika.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naye mfalme atafanya kama apendavyo; naye atajitukuza na kujiadhimisha juu ya kila mungu, naye atanena maneno ya ajabu juu ya Mungu wa miungu, naye atafanikiwa mpaka ghadhabu itakapotimia; maana yaliyokusudiwa yatafanyika.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mufalme atafanya kama anavyopenda. Atajitukuza na kujivuna kwamba yeye ni mukubwa kuliko miungu yote, na kumutukana Mungu wa miungu. Ataendelea kufanikiwa mpaka kasirani ifikie ukomo wake, maana yaliyopangwa sherti yatimie.