Daniel 11:38 — Compare Translations
9 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Badala ya miungu hiyo atamheshimu mungu mlinzi wa ngome, ambaye wazee wake kamwe hawakumwabudu, atamtolea dhahabu, fedha na vito vya thamani, na zawadi za thamana kubwa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Badala ya kuwajali miungu, ataheshimu mungu wa ngome; mungu ambaye hakujulikana na baba zake ndiye atamheshimu kwa dhahabu na fedha, kwa vito vya thamani, na zawadi za thamani kubwa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini katika mahali pake atamheshimu mungu wa ngome; na mungu ambaye baba zake hawakumjua atamheshimu, kwa dhahabu, na fedha, na vito vya thamani, na vitu vipendezavyo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Badala ya miungu hiyo atamheshimu mungu mlinzi wa ngome, ambaye wazee wake kamwe hawakumwabudu, atamtolea dhahabu, fedha na vito vya thamani, na zawadi za thamana kubwa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Badala ya kuwajali hao miungu, ataheshimu mungu wa ngome, mungu ambaye hakujulikana na baba zake, atamheshimu kwa dhahabu na fedha, kwa vito vya thamani na zawadi za thamani kubwa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Badala ya kuwajali miungu, ataheshimu mungu wa ngome; mungu ambaye hakujulikana na baba zake ndiye atamheshimu kwa dhahabu na fedha, kwa vito vya thamani na zawadi za thamani kubwa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mahali pao atamheshimu mungu wa maboma nao mungu, baba zake wasiyemjua, atamheshimu kwa kumtolea dhahabu na fedha na vito na vitu vingine vipendezavyo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini katika mahali pake atamheshimu mungu wa ngome; na mungu ambaye baba zake hawakumjua atamheshimu, kwa dhahabu, na fedha, na vito vya thamani, na vitu vipendezavyo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Pahali pa miungu hiyo atamuheshimu mungu mulinzi wa kuta za muji, ambaye babu zake hawakumwabudu hata kidogo. Atamutolea zahabu, feza na mawe ya bei kali, na zawadi za bei kubwa.