Daniel 11:39 — Compare Translations
9 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Atazishughulikia ngome zake kwa msaada wa mungu wa kigeni. Wale wanaomtambua kuwa mfalme, atawatunukia heshima kubwa, atawapa vyeo vikubwa na kuwagawia ardhi kama zawadi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Atashambulia ngome zenye nguvu mno kwa msaada wa mungu wa kigeni, naye atawaheshimu sana wale watakaomkubali yeye. Atawafanya watawala wa watu wengi, na atagawa nchi kwa gharama.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naye ataziteka nyara ngome zenye nguvu kwa msaada wa mungu mgeni; na yeye atakayemkubali atamwongeza kwa utukufu; naye atawapa kumiliki wengi; naye ataigawa nchi kwa rushwa,
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Atazishughulikia ngome zake kwa msaada wa mungu wa kigeni. Wale wanaomtambua kuwa mfalme, atawatunukia heshima kubwa, atawapa vyeo vikubwa na kuwagawia ardhi kama zawadi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Atashambulia ngome zenye nguvu mno kwa msaada wa mungu wa kigeni naye atawaheshimu sana wale watakaomkubali yeye. Atawafanya watawala juu ya watu wengi na atagawa nchi kwa kulipia.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Atashambulia ngome zenye nguvu mno kwa msaada wa mungu wa kigeni naye atawaheshimu sana wale watakaomkubali yeye. Atawafanya watawala juu ya watu wengi, na atagawa nchi kwa gharama.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Katika miji yenye maboma atafanya hivyo kwa ajili ya huyo mungu mgeni: atakayemwungama atampa macheo mengi, tena atampa watu wengi kuwatawala, nayo nchi atamgawia kuwa malipo yake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naye ataziteka nyara ngome zenye nguvu kwa msaada wa mungu mgeni; na yeye atakayemkubali atamwongeza kwa utukufu; naye atawapa kumiliki wengi; naye ataigawa nchi kwa rushwa,
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Atazishugulikia kuta za muji wake kwa musaada wa mungu wa kigeni. Wale wanaomutambua kuwa mufalme, atawaongezea heshima kubwa, atawapa vyeo vikubwa na kuwagawanyia inchi kama zawadi.